Brighton Masalu
KIJANA aliyefahamika kwa jina la Abdul Kiba
amejikuta katika wakati mgumu baada ya
kukamatwa akiwa na simu inayodaiwa kuwa
ni ya wizi na ‘ kuswekwa’ sero kufuatia
jitihada za ndugu zake kumuwekea
mdhamana kugonga mwamba , Ijumaa
limetonywa.
Abdul Kiba.
Tukio hilo lilijiri Jumanne ya wiki hii katika
viwanja vya Karume jijini Dar , wakati kijana
huyo alipokuwa akicheza mpira.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini
kilichokuwa uwanjani hapo , muda mfupi
baada ya mchezo huo kumalizika , ndipo
Abdu akawekwa chini ya ulinzi wa polisi wa
kituo cha Msimbazi , kwa tuhuma ya kuwa
na simu ya wizi aina ya Samsung Galaxy
yenye thamani ya shilingi laki nane, ambayo
inadaiwa kuwa mali ya mfanyabiashara
aliyetajwa kwa jina la Abdallah Muhidini .
Katika mahojiano yake na Polisi, Abdul
alijitetea kuwa simu hiyo aliuziwa na vijana
wawili siku za hivi karibuni aliowataja kwa
majina ya Shaaban Rajab au Kibabu kama
anavyojulikana kwa wengi ( anayeshikiliwa na
polisi ) .
Hata hivyo licha ya utetezi huo , Abdul
alifunguliwa kesi jalada Na. MS /
RB/12267 /2013 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya
simu, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi wa Ilala, ACP Juma Bwire alithibitisha
kukamatwa Abdul Kiba na kwamba upelelezi
bado unaendelea .
Thursday, December 5, 2013
ABDU KIBA MBARONI KWA SIMU YA WIZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kununua simu mkononi shida
ReplyDelete