Friday, December 6, 2013

AZAMTV YAPATA LESENI YA KUWA HEWANI RASMI


TCRA yaipa Azam Media leseni kuiwezesha
kuendesha shughuli zake.
Azam Media Ltd leo imepata leseni kutoka
Mamlaka ya Mawasilino Tanzania ( TCRA ) na
hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi
shughuli zake hapa Tanzania .
Hatua hii muhimu sasa inaiwezesha AzamTV
kuanza kutoa huduma zake kwa wateja wake
kote Tanzania kuanzia tarehe16 Desemba .
Huduma hii itwapa fursa wateja kuangalia
zaidi ya chaneli 50 za kitaifa na kimataifa
ziliozosheheni burudani kwa ajili ya familia
kwa bei nafuu ya shilingi 12 ,500 /= kwa
mwezi. Kutakuwepo wigo mpana wa
kuchagua kifaacho kuangalia vikiwemo vipindi
vya michezo , makala , watoto na tamthilia
kutoka Tanzania , barani Afrika na sehemu
mbalimbali za dunia . Baadhi ya vipindi hivyo
tajwa vitapatikana katika chaneli maarufu
kama vile National Geographic Gold na
Nickelodeon, na pia matangazo yetu
yatakuwa na chaneli za bila malipo zikiwemo
TBC 1, Channel 10, Clouds , ZBC na K24 .
Jambo la kusisimu zaidi ni kwamba
AzamTV itakuwa na matangazo katika
chaneli zake tatu :
AzamOne - Itakuwa na vipindi vya kiafrika ,
ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu
masuala ya Afrika Mashariki kwa lugha ya
Kiswahili . Hii ndiyo chaneli ambayo itakuwa
ikirusha matangazo ya Ligi Kuu ya soka
Tanzania Bara ;
AzamTwo – Hapa vitapatikana vipindi vya
burudani kwa familia amabavyo ni vya
kimataifa na baadahi ya hiovyo vitakuwa
katika lugha ya kiswahili ;
SinemaZetu – Chaneli maalum kwa ajili ya
tamthilia za kitanzania .
Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys
Torrington , alisema : “Huu ni wakati wa
kujivunia kwa Tanzania kwani sasa ina
huduma za luninga zinazopatikana kwa bei
ambayo wengi wanaweza kuimudu . Miezi
michache ijayo tutaivusha huduma hii mipaka
hadi katika nchi zingine za Afrika Mashariki
na hata mbali zaidi . Nimefarijika kwamba
tumewekeza vilivyo katika chombo hiki cha
kitanzania na tutaendelea kufanya hivyo ”.
Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja
ambao hawatapenda kungojea kuzinduliwa
rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya
ofisi zake za Dar es Salaam itakuwa wazi
kuanzia leo ( Ijumaa Desemba 6, 2013 ) .
Wateja wataweza kununua vifaa muhimu
kutoka duka la AzamTV na kwa mawakala
walioidhinishwa na hivyuo kuweza kujionea
vipindi mbalimbali kuanznia sasa – japo
malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia
Desember 16.

1 comment:

.