Thursday, December 5, 2013

BAUNSA ADAIWA KUUA KWA RISASI


Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
KIJANA aliyefahamika kwa jina moja la
Andrew , mkazi wa Yombo , jijini Dar
amedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na
mlinzi ‘ baunsa’ wa Kampuni ya Harvest
Public Action iliyopewa dhamana ya kuuza
nyumba na Benki ya BOA .
Marehemu Andrew enzi za uhai wake.
Kikizungumza na Ijumaa hivi karibuni , chanzo
makini kilidai Endrew alifika na pikipiki katika
eneo la nyumba moja iliyopo Temeke mtaa
wa Uwanja wa Taifa , Kata ya Mgulani ,
Wilaya ya Temeke yenye kitalu namba KT/
MBR /BS/47 kwenda kushuhudia mnada huo
ndipo alipopigwa risasi.
Chanzo kilidai kuwa , mnada huo ulikuwa ni
kwa ajili ya kuuza nyumba ya marehemu
Thabit Tibwa ambapo Endrew aliagizwa na
bosi wake akaangalie inauzwa bei gani.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Andrew .
Ilidaiwa , nyumba hiyo ilikuwa kwenye
mgogoro ambapo baba mdogo wa watoto wa
marehemu ambaye ndiye msimamizi wa
mirathi aliyetambulika kwa jina moja la
Robert, alichukua mkopo katika Benki ya BOA
huku akiandika nyumba hiyo kama dhamana
yake, akashindwa kulipa .
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa , baada
ya kijana huyo kufika eneo la mnada ,
yalitokea majibizano kati ya wauzaji na
baadhi ya wateja waliojitokeza na baunsa wa
kampuni hiyo alidaiwa kumpiga risasi Andrew
na kusababisha kifo chake .
“Walimpiga risasi, akafariki palepale huku
watu wengine wakikimbia kuokoa maisha
yao,” kilisema chanzo hicho bila kufafanua
zaidi chanzo cha mabishano hayo.
Andrew baada ya kupigwa risasi .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo , Vincent
John, alisema siku hiyo akiwa ofisini kwake,
walifika vijana wawili waliomletea barua ya
kumpa taarifa juu ya mnada huo.
“Tuliwaambia nyumba hiyo ni ya watoto na
ina mgogoro ambao umefikishwa
mahakamani na kesi yake ingeanza
kusikilizwa Jumatatu ya Desemba 2, lakini
wao walisema hiyo haiwahusu na ndipo
yakatokea hayo, ” alisema mwenyekiti huyo na
kuongeza :
“Tulitoka na kushuhudia maiti na tulipouliza
kulikoni wale mabwana wa Harvest waliingia
kwenye gari na kukimbiza gari lao, hata hivyo
tulipokwenda Kituo cha Polisi Chang ’ ombe ,
tuliwakuta wameshajisalimisha mikononi
mwa polisi na kusema wameua kwa bahati
mbaya walipokuwa wakijihami .”
Diwani wa mtaa huo , Juma Mkenga alisema
amesikitishwa na tukio hilo na kuiomba
serikali ihakikishe inakusanya silaha kwa
watu wasiokuwa na vigezo vya kumiliki
silaha hizo kwani mauaji ya silaha yamezidi
kushamiri kila kukicha .

1 comment:

  1. Tanzania kama ulaya unamiliki tu silaha unaua ukizinguliwa

    ReplyDelete

.