Mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha 100.5
Times Fm, Gardner G. Habash aka Captain
ameelezea jinsi anavyomkumbuka rais wa kwanza
mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Captain G. Habash ameiambia tovuti ya Times
Fm kuwa aliwahi kulitembelea gereza alilofungwa
Mandela , Robben Island huko Afrika Kusini, na
kushuhudia chumba alichokua akishikiliwa.
“Nimewahi kutembea South Africa na nikafika
kwenye mji wa Cape Town, na kule niliwahi
kutembelea sehemu moja ambayo ni gereza la
Robben Island, alipowahi kufungwa na kushikiliwa
Nelson Mandela kwa muda mrefu sana. Pale
nilipata nafasi ya kuona kile chumba ambacho
alikuwa akilala Mandela, na mazingira magumu
ambayo alikuwa akiishi,” amesimulia Gardner.
“Tulipata hadithi pia ya jinsi ambavyo alikuwa
akiteseka katika harakati za kufanya ukombozi
wa kupigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.”
Gadner amesema pamoja na kushuhudia sehemu
ya mazingira magumu na kusimuliwa mateso
aliyoyapata Mzee Mandela, alishangaa kuona
baada ya kutoka alikubali kusamehe na kusahau.
“Lakini kitu kikubwa ambacho nilistaajabu ni vile
ambavyo alipitia Mandela, lakini baada ya kutoka
akakubali kusamehe na kusahau kila kitu na
kuunda taifa moja lenye manufaa kwa wa-South
Africa wote, taifa ambalo aliliita Rainbow Nation
kwa maana kwamba ni taifa la watu wa rangi
zote. Taifa ambalo litakuwa ni kwa ajili ya wa-
South Afrika pamoja na maslahi ya wa-South
Africa,” ameongeza Gardner.
Amesema matendo ya Mandela yanamtofautisha
na viongozi wengine wengi duniani, na kwamba
anaamini kwamba yeye ndiye kiongozi bora zaidi
kwa karne hii, mwenye hekima, busara pamoja na
karama ya Mwenyezi Mungu.
“Naungana na South Africa, Afrika nzima pamoja
na dunia kutoa heshima zangu kwa Mzee Nelson
Mandela pamoja na familia yake.”
Saturday, December 7, 2013
Exclusive: Gardner Habash aelezea jinsi alivyokishuhudia chumba cha gereza alipofungwa Mandela
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hee! Nae huyu
ReplyDelete