SIKU chache baada ya kuingia katika
mgogoro na msanii mwenzake , Chuchu Hans
kwa madai ya kugombea penzi la Vincent
Kigosi ‘ Ray ’ , muigizaji Blandina Chagula
‘ Johari’ amesema amegundua mapenzi
yanaumiza na ni sumu mbaya maishani .
Blandina Chagula ‘ Johari’ .
Akizungumza na mwandishi wetu mwishoni
mwa wiki iliyopita katika moja ya mahojiano
maalumu, Johari alisema mapenzi si kitu cha
kuendekeza kwani ni hatari na ndiyo maana
baadhi ya watu hufikia hatua ya kuchukua
uamuzi mgumu wa kujiua .
“Mapenzi ni kitu kingine kabisa , sikuwahi
kujua ni kwa nini baadhi ya watu hufikia
hatua ya kukatisha maisha yao kisa mapenzi ,
hakika mapenzi ni sumu kali sana maishani
usipojiongoza, ” alisema Johari.
Thursday, December 5, 2013
JOHARI AKIRI MAPENZI KUWA SUMU YA MAISHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huyi mwandishi alikua anataka kujaza nafasi
ReplyDelete