KAULI aliyoitoa msanii nyota wa filamu
Bongo, Elizabeth Michael ‘ Lulu’ kuhusu
kupima mara kwa mara maambukizi ya
ugonjwa hatari wa Ukimwi , imeibua utata
mkubwa miongoni mwa wadau wakihoji ana
nini moyoni mwake ? Amani limeelezwa .
Katika tamasha maalum la Siku ya Ukimwi
Duniani lililofanyika Desemba Mosi, mwaka
huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar , Lulu akiwa miongoni mwa
waliohudhuria , alikiri kupima virusi vya
ugonjwa huo mara kwa mara na kuwataka
vijana wengine waige mfano wake.
“Vijana wengi waoga kujitokeza kupima
Ukimwi, wanadhani kwa kufanya hivyo ni
kujitafutia hofu ya kifo kitu ambacho si kweli .
“Hata mimi nilikuwa muoga sana lakini
baada ya kupata elimu stahiki juu ya
umuhimu wa kujua afya kila mara , nimekuwa
nikipima mara kwa mara , hivyo hata ninyi
nawaasa mjenge tabia ya kupima Ukimwi
mara kwa mara, ” alisema Lulu.
Baadhi ya wadau walihoji kulikoni msanii
huyo mwenye historia mbaya huko nyuma,
hasa ya starehe awe na tabia hiyo ya kupima
Ukimwi mara kwa mara?
Wengi walihoji je amekuwa akipima mara
kwa mara kwa sababu huwa anabadilisha
wanaume mara kwa mara ? Wengine walihoji
amekuwa hatumii kinga?
“Kwa nini amekuwa na tabia ya kupima
Ukimwi mara kwa mara? Ina maana huwa
hatumii kinga? Au ni uaminifu mdogo katika
uhusiano?” alihoji mdau mmoja ambaye pia
ni msanii mkubwa wa filamu za Kibongo
akiomba kusitiriwa jina.
Juzi paparazi wetu alilazimika kumsaka Lulu
ili azungumzie kwa kina juu ya mjadala huo
lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Wednesday, December 4, 2013
LULU ANA NINI?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mmmh, huyo ni kicheche ndo maana anapima pima kila mara
ReplyDelete