JINA KAMILI: Nelson Rolihlahla Mandela
A. K .A : Mandela
MAJINA YA UTANI : Madiba , Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA : Mveso , Transkei ,
South Africa
KAZI : Mwanaharakati , Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA : Julai 18 , 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05 , 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South
Africa
ELIMU : Taasisi ya Clarkebury , Chuo cha
Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare ,
Chuo Kikuu cha London , Chuo Kikuu cha
Witwatersrand, Johannesburg .
ASILI YAKE
Nelson Mandela , Mwanasiasa maarufu nchini
Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye
alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza
ubaguzi wa rangi nchini mwake , ni mtoto wa
Chifu wa kabila la Tembu , Chifu Henry
Mandela. Mandela alizaliwa katika mji mdogo
wa Transkei .
CHAMA CHA ANC
Mandela alisoma katika Chuo Kikuu cha Fort
Hare na Chuo Kikuu cha Witwatersrand .
Akawa mwanasheria mwaka 1942 . Mwaka
1944, alijiunga na Chama cha ANC , chama
kilichodhamiria kuutokomeza utawala wa
makaburu weupe pekee. Mwaka 1960 , Chama
tawala cha makaburu kilikipiga marufuku cha
cha ANC na kuwashitaki viongozi wake kwa
kosa la uhaini, lakini Mandela aliachiwa huru.
Rais Barack Obama akiwa ndani ya chumba
cha gereza alimokuwa akiishi Mandela
akitumikia kifungo chake cha maisha .
KUFUNGWA GEREZANI
Akiendeleza harakati zake za kupambana na
makaburu, Mandela alikamatwa , akatiwa
hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha
gerezani kuanzia mwaka 1964 hadi 1990 ,
ambapo maisha yake kama kiongozi wa
harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi
yakajulikana dunia nzima. Kama mfungwa wa
dhamiri, Mandela mara kwa mara alikataa
kuachiwa kwa masharti .
Mandela akiwa ndani ya chumba cha gereza
alimokaa kwa miaka 26 , hapa alikwenda
kutembea baada ya kuwa rais .
KUACHIWA HURU
Mwaka 1990 , akiwa amekaa jela kwa miaka
26 na akiwa na umri wa miaka 71, iliachiwa
huru bila masharti yoyote baada ya utawala
wa kibaguzi kushinikizwa na jumuiya ya
kimataifa. Mwaka 1993 , Nelson Mandela
alishinda Tuzo ya Nobel kwa harakati zake
za kisiasa .
Nelson Mandela akiwa na binti yake
Princess Zenani Dlamini ( kati ) wengine ni
wajukuu zake Zaziwe Manaway , ( kushoto
aliyembeba kitukuu chake Ziphokazi
Manaway ) na Zamaswazi Dlamini ( kulia ,
mwenye kitukuu Zamakhosi Obiri ) .
MAISHA YA URAIANI
Mwaka 1994 akiwa katika umri huo, Mandela
aligombea kiti cha uraisi na kushinda akiwa
raisi wa kwanza mweusi .
Thursday, December 5, 2013
NELSON MANDELA : HISTORIA YA KUSISIMUA YA MAISHA YAKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment