Thursday, December 5, 2013

RAY AIPASUA BONGO MOVIE


Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘ Ray ’
anadaiwa kulipasua Kundi la Bongo Movie
kutokana na uchaguzi wa kundi hilo
unaotarajiwa kufanyika leo katika Viwanja
vya Leaders, Kinondoni jijini Dar , Ijumaa lina
habari kamili .
Vincent Kigosi ‘ Ray ’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya
wasanii wa filamu wanaounda kundi hilo
wanadai Ray hafai kuliongoza kutokana na
skendo ya kuwagonganisha mademu
inayomtafuna huku wengine wakimuunga
mkono.
“Kuna baadhi yetu wamekuwa wakikaa vikao
ili kutaka kumweka pembeni Ray kwa kuwa
ameshindwa kuleta umoja ndani ya Bongo
Movie na amekuwa akifanya mambo
yasiyokubalika…” alisema mmoja wa wasanii
ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini .
Chanzo hicho kimesema kwamba wasanii
wasiomtaka Ray wamekuwa wakiweka vikao
usiku katika kumbi mbalimbali za burudani
za jijini Dar kwa ajili ya kumng ’ oa kwenye
cheo hicho.
Wasanii wanaomkubali Ray wanadai
anastahili kuendelea kuliongoza kundi hilo
kwa kuwa ana msimamo thabiti na hakuna
mwingine anayeweza kuliongoza.
Msanii wa filamu za Kibongo, Steven
Mengere ‘ Steve Nyerere , amesema uongozi
wa Ray unafika kikomo na wanatakiwa
kumchagua kiongozi mpya au kuendelea
naye na jukumu hilo liko mikononi mwa
wasanii wenyewe.
“Kimtazamo Bongo Movie linaenda vibaya na
hii siyo kwa sababu ya Ray , bali wasanii
wote ni jukumu letu kulijengea heshima kundi
hilo, katika uchaguzi wa leo Ray anaweza
kuchaguliwa au asichaguliwe kwani kura ni
demokrasia …” alisema Steve Nyerere .
Ray hakuweza kupatikana mara moja
kuuzungumzia mpasuko huo ndani ya Kundi
la Bongo Muvi .

2 comments:

  1. NGOJA NIMSHAWISHI WASTARA AGOMBANIE HIYO NAFASI

    ReplyDelete
  2. Heeheeeee mi yangu machooo bongo movie wanamamboo kweli bongo movie woote wapuuzi na wanafanya upuuzi

    ReplyDelete

.