Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza kuwa
katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote
zitapepea nusu mlingoti nchi nzima.
Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo
kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia
kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia
salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa
Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi
Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi
wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee
Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba,
2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba
mkubwa kwetu sote.”Afrika ya Kusini, Afrika na
dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na
shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na
21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi
wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi
shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na
mstahimilivu”. Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni
kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa
moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo
uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa
Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya
kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi
wa rangi.
“Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi
binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni
wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia
kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo,
kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na
wananchi wenzake”. Rais ameongeza kusema,
“Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze
roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema
peponi”.
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na
umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza
Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa
ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa
miaka 27. Mandela alikuwa anatibiwa homa ya
mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa
hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini,
Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga
lakini yuko mahali salama. Rais Zuma amesema
kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama
mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya
Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika
sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika
Kusini baada ya kutoka gerezani.
Friday, December 6, 2013
TANZANIA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA NELSON MANDELA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
R.I.P SIMBA WA AFRIKA NELSON MANDELA
ReplyDeleteMpe hi bi mkubwa afu mwambie nyerer bongo hajira nomaa
ReplyDelete