Je ni kweli Steven Kanumba ameondoka na Kila
kitu?
Tangu Alipofariki Tasnia ya filamu Tanzania ni
kama imelala usingizi wa Pono, Potelea mbali
hata kama kuna watu bado wanaingiza mamilion
ya pesa lakini ukweli ni kwamba mvuto wake
unaendelea kupotea ..Nani anabisha?
Kwa kudhihirisha hilo Tazama wasanii wa kike
wanavyojiingiza kwenye fani zingine
zinazolipa ..Hawataki tena kupaka poda za
location bali wanataka kukata viono kama Ray
Majukwaanii...Mabadiliko na Maisha ya Shilole
na Snura ni Mfano Tosha kabisa..
Kanumba alikuwa ni kila kitu biashara ya Filamu
ilifanyika kupitia yeye..mzunguko wa soko
uliundwa kupitia kanumba..Alisafiri kutoka
mashariki kwenda magharibi, kaskazini na kusini
kwa sababu ya tasnia ya filamu tu hakuwa
akisafirisha Unga wala Pembe za ndovu..
Hivi sasa wasanii wa filamu hawavumi kupitia
kazi zao, Ukimtazama mtu kama Ray utagundua
kazi zake zilikuwa zinavuma kwa msukumo wa
Ray lakini sasa zote chali ...Sasa anavuma kwa
kugonganisha vimwana badala ya kuingiza
movies mpya mtaani...
Kinacho Imaliza Bongo Movies kwa sasa ni
Ubinafsi, Haraka , Mipango Butu na Tamaaaaa....
This is Wake up Call...
Thursday, December 5, 2013
TASNIA YA BONGO MOVIES CHALI-KANUMBA ALIONDOKA NA KILA KITU-SASA WAMEBAKI KUHAHA NA KUBADILI FANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment