Sunday, February 23, 2014

LIJUE JINA LA MBUNGE WA KATIBA ALIYELILIA KUPEWA I-PAD BUNGENI


Mjumbe wa katiba alielilia Ipad
Bungeni amefahamika kwa jina la Suleiman
Nchambi na hii ndio kauli yake.Ninamnukuu
kama ifuatavyo;
"Dunia ya sasa imegubikwa na utandawazi
ambao kuanzia shule za msingi wanatumia
Laptop,sasa ningependa Ipad, ilikupunguza
gharama zinazotumika na Bunge kuchapisha
nyaraka mbali mbali".
"Lazima wanafunzi wa shule na vyuo wajifunze
kutoka kwetu,sasa wanatushangaa tukiendelea
kutumia utaratibu huu wa kugawiana
makaratasi yenye nyaraka litakuwa jambo la
kusikitisha,nina imani tukipatiwa vifaa hivyo
watendaji watakuwa wanatutumia ujumbe wa
taarifa tunazopaswa kujadili au kazi
tulizopangiwa kufanya," alisema.
Hata hivyo,mwenyekiti wa muda wa Bunge
hilo,mh.Kificho alipinga wazo hilo kwa maelezo
kuwa utaratibu huo ni wa gharama zaidi.
CHANZO:Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

.