MAMA wa Miss Tanzania 2006 aliye pia staa
wa muvi za Bongo , Wema Sepetu, Mariam
Sepetu amesema anamwomba Mungu bintiye
huyo amfumanie mpenzi wake asiyemkubali,
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ,
Amani lina picha kamili.
Wema na Diamond.
Akizungumza na mapaparazi wetu juzikati
jijini Dar es Salaam, mama Wema alisema:
“Najua kwa sasa sina tena mamlaka ya
kuingilia mapenzi ya binti yangu kwani
mambo hayo yamenichosha , yananiumiza na
kichwa .
“Lakini naomba sana kwa Mungu itokee siku
moja Wema amfumanie Diamond akiwa na
mwanamke mwingine labda ndiyo itakuwa
kikomo chao cha kuwa wapenzi kwani ndiyo
ndoto ninayoiota kila siku. ”
KWA NINI ANAOMBA DUA BAYA ?
Mama Wema alikwenda mbele zaidi kwa
kusema kwamba, amegundua binti yake
huyo hana ubavu wa kuachana na Diamond
hata kama atasikia ana mwanamke
mwingine.
Mama Wema , Mariam Sepetu.
MAGAZETI PIA YAMESHINDWA
Mwanamke huyo anayemwogopa Mungu tu,
alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwamba,
kuna wakati baadhi ya magazeti pendwa
nchini yaliandika Diamond kuwa na demu
mwingine lakini Wema hakukasirika wala
kuachana na staa huyo wa muziki wa kizazi
kipya .
MSIKIE MWENYEWE
“Kwa hiyo mchezo mzuri ni yeye ( Wema )
kumfumania huyo Diamond wake , maana
magazeti tu kuandika kwamba ana
uhusiano na mwanamke mwingine mwanangu
alivyofanywa mjinga wa kutupwa ,
hatamwacha.
“Mimi najua Wema anashindwa kukaa
chonjo kwa sababu ndumba zimemtawala,
amefunikwa labda baadaye atafunguka , ”
alisema mama Wema .
AIGUSA SAFARI YA DIAMOND NCHINI
NIGERIA
Mama Wema akaanika jambo ambalo
halijawahi kujulikana kabla .
Alisema : “ Huyo Diamond ndo maana
alikwenda Nigeria akashindwa kupiga
muziki kwa sababu hakwenda na Wema ,
sasa ameona ampumbaze ili aweze kwenda
naye nchi za nje kwa masilahi yake binafsi,
ataishia kumuahidi tu hana uwezo wa
kumnunulia Wema kitu chochote chenye
thamani kubwa, ni mpenda misifa tu.
“Si mnamjua huyo ni mtoto wa Tandale?
Anajiita yeye m.. .( alitaja jina la kinyesi )
na kweli yuko hivyo .
NDUGU WA DIAMOND WAMEJAZANA KWA
WEMA
“Ndugu zake walivyo washamba wamejazana
hovyo pale kwa Wema . Wajinga mno, maana
mshamba siku zote ni mshamba , ” alisema
mama huyo .
HATAKI KUSIKIA WEMA ANA MIMBA YA
DIAMOND
Katika hali iliyoonesha kwamba kweli
hampendi Diamond, Bi . Mariam alisema
hataki kusikia binti ana ujauzito wa msanii
huyo .
Alisema : “ Mbegu ( uzao) gani atakayoileta
kwangu, huyo mjukuu si atakuwa balaa ,
siwezi kuharibiwa wajukuu . Mtoto
asiyeeleweka siwezi kumshika.”
Wema .
ACHIMBA MKWARA
“Halafu nataka kuwaambia enyi watu wa
magazeti, haya mambo ya kumwongelea
huyo domo acheni mara moja , dunia
itamnyoosha, ” alisema.
AJIRUDI KWA MWANAYE
Mama Wema alisema hawezi kumlaumu sana
binti yake kwa vile akili si yake, yeye
(Wema ) ni mwanake na atabaki kuwa
mwanamke , ila siku zote lenye mwanzo
halikosi kuwa na mwisho .
DIAMOND SASA
Juzi , Amani lilimtafuta Diamond kwa njia
ya simu na kumjulisha kuhusu ndoto za
mama mkwe wake huyo ambapo aliishia
kucheka.
“Teh ! Teh ! Teh ! Thubutu. ”
Diamond.
HAIJAWAHI KUTOKEA
Kumbukumbu za makabrasha ya Amani
zinaonesha kwamba , katika historia ya
wapenzi wa Wema , mzazi huyo hakuwahi
kutokea kumkubali Diamond hata siku moja
tu.
Amekuwa akimshukia mara kwa mara ,
madai yake siku zote ni kwamba , katika
maono yake hajawahi kuona mapenzi ya
kweli ya Diamond kwenda kwa Wema .
Japokuwa pia hajawahi kusema kama kuna
mapenzi ya kweli ya Wema kwa Diamond.
Wema amewahi kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na marehemu Steven Kanumba ,
Jumbe Yusuf, Chalz Baba na Clement ‘kigogo
wa ikulu ’ . Pia amewahi kudaiwa kutembea
na TID na Mr Bluu.
Thursday, February 20, 2014
MAKUBWA ! MAMA WEMA AKESHA AKIOMBA DIAMOND AFUMANIW
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mapenzi penzi mama wema awe mpole tu mwanae asikii
ReplyDelete