Na Jelard Lucas
MISS Tanzania mwaka 2011, Salha Israel
amevunja ukimya baada ya kumuweka wazi
mwanaume anayetoka naye , jambo ambalo
amejaribu kulifanya siri kwa muda mrefu.
Miss Tanzania mwaka 2011, Salha Israel .
Salha alifungua kinywa na kubainisha hayo,
hivi karibuni alipokuwa kwenye mahojiano
na
inayorushwa na mtandao namba moja wa
burudani Bongo, www. globalpublishers.info
ya Kampuni ya Global Publishers .
Akijibu swali la mtangazaji aliyekuwa
akifanya naye mahojiano , Luqman Maloto ,
aliyetaka kujua kuhusu uhusiano wake ,
Salha alijibu kwa kifupi akisema : “ Yeah!
Ninaye mchumba .”
Akaongeza: “Anaitwa Moses. Ndiye moyo
wangu, maisha yangu , kila kitu kwangu .
Nafurahi mwanaume huyu kuja maishani
mwangu, maana amekamilisha ndoto zangu .
Najivunia kuwa naye kwa kweli .”
Hata hivyo , hakutaka kufafanua zaidi
kuwa huyo Moses ni nani , anafanya nini na
jina lake la pili , kwa maelezo kuwa ni
mapema kufanya hivyo .
Huyu hapa anafafanua zaidi : “ Hiyo
inatosha , ni Moses. Hakuna haja ya
mwanaume yeyote kuwaza tena kuhusu
mimi. Nafasi imejaa. ”
“Nawashukuru sana G lobal TV kwa kunipa
nafasi ya kutoa yangu ya moyoni hasa
katika kuweka mambo yangu hadharani ,
najipanga vizuri kufanya mambo makubwa
ya kijamii na siyo skendo kama watu
wanavyochukulia , ” alisema Salha ambaye
kwa sasa ametia maguu kwenye tasnia ya
filamu za Kibongo .
Nje ya uhusiano , Salha amezungumza mengi
kuhusu filamu , maisha ya warembo na
mengineyo
Thursday, February 20, 2014
MISS TANZANIA AMWANIKA MCHUMBA WAKE !
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment