Wednesday, February 12, 2014

WAZOZANA GEREZANI

MAISHA ya uraiani baada ya kutoka
gerezani ndiyo mzozo uliopo sasa kati ya
wanamuziki mahiri nchini ambao ni baba na
mwana, Nguza Vicking ‘Babu Seya ’ na
Johnson Nguza ‘ Papii Kocha’, Amani
limetonywa.
Nguza Vicking ‘Babu Seya ’ na Johnson Nguza
‘ Papii Kocha’ wakitoka Mahakamani .
Chanzo makini kimesema kuwa wawili hao
wamefikia hali hiyo baada ya kila mmoja
kuanika dira ya maisha yake ya uraiani
baada ya kuachiwa kutoka katika kutumikia
kifungo cha maisha jela katika Gereza la
Ukonga.
MAISHA YAO YANAPISHANA
Kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa Papii
Kocha aliulizwa na baba yake maisha yake
ya uraiani yatakuwa ya aina gani ambapo
bila kupepesa macho alisema atarudia kazi
ya muziki kama zamani .
“Ishu kubwa ni maisha ya uraiani , Papii
amemhakikishia baba yake kwamba akiwa
uraiani ataendelea na muziki jambo ambalo
Babu Seya hakubaliani nalo hata kidogo , ”
kilisema chanzo cha ndani .
Kikaendelea : “ Unajua yule mzee (Babu
Seya) yeye anaamini kwamba uraiani lazima
wabadili staili ya maisha kwa vile kuwa
kwao huru kuna mkono wa Mungu kwa hiyo
kuendelea kuishi maisha ya kidunia ni
kutorudisha shukurani kwake.”
Nguza Viking ‘Babu Seya ’ ( wa pili kulia ) na
mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ ( wa
pili kushoto ) wakiwa mahakamani.
MSIMAMO WA BABU SEYA
Wakati Papii Kocha akianika msimamo huo
kwa baba yake ambao ulisababisha
wazozane, mzee huyo yeye ameweka wazi
kwamba maisha yake ya uraiani ni ya
kumtumikia Mungu mwanzo mwisho .
“Lakini Babu Seya alimlaumu sana mwanaye
kwamba kuendelea kufanya mambo ya
duniani ni kutomtendea haki Mungu kwa
vile nguvu zake ndiyo mwanga wa maisha
yao mapya , ” kilisema chanzo.
HAYA YOTE YAMEKUJAJE?
Chanzo kilisema mambo hayo yote
yameibuka kufuatia rufaa zote za
wafungwa hao kupigwa chini na hivyo
hatima yao kuwa mikononi mwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ‘ JK’
ambapo wanaamini wapo huru tayari
kinachosubiriwa ni siku tu .
Chanzo: “Unajua imani ni kitu cha ajabu
sana. Yeye ( Babu Seya) anachoamini wapo
huru tayari , ila siku ndiyo ya kuvutia subira
lakini pia anaamini mbali na msamaha wa
JK, Mungu anatenda. ”
BABU SEYA ATATUA KANISA LA LIFE IN
CHRIST
Dodosa zaidi za ndani zinaweka wazi
kwamba, msimamo wa Babu Seya kwa
maisha ya uraiani ni kuabudu kwenye
Kanisa la Life in Christ Ministries ( Zoe)
lililopo Tabata Segerea jijini Dar ambako
ndiko anakotoa huduma mtoto wake
aliyeachiwa huru katika kesi hiyo na
Mahakama ya Rufaa Tanzania , Nguza
Mbangu.
Babu Seya na Papii Kocha wakiwa nje ya
mahakama .
NGUZA MBANGU AONGEA NA AMANI
Baada ya taarifa zote hizo , juzi Amani
lilimtafuta Nguza Mbangu ili kumsikia
alichonacho kuhusu maisha ya baba yake
uraiani, hasa suala la kuokoka na
kumrudia Mungu.
Mbangu: “ Suala la kuokoka ni la Mungu
mwenyewe akiamua kumvuta mtu. Kama nia
ya moyo wake ni hiyo basi ina maana mzee
(baba ) ameshavutwa .
“Kwanza nataka nikwambie kitu Ndauka ,
siku zile baba na Papii waliposhindwa rufaa
magazeti yaliandika sana , ooooh! Babu
Seya na mwanaye kufia jela . Mimi
nakwambia hivi, suala la baba na Johnson
(Papii ) watu wamekuwa wakiliangalia
kimwili .
“Mimi ninachojua wale wapo huru hata leo
hii ( juzi Jumanne) , nilishakwambia siku za
nyuma na leo narudia tena , Tanzania
itamshangaa sana Mungu kupitia wale watu
(Babu Seya na Papii ).
“Tena nakuahidi kwamba , siku si nyingi,
pengine mwezi huuhuu . Yaani , sijui
nikwambiaje, nitakupigia simu, nadhani
keshokutwa ( leo Alhamisi ), ndipo utajua
nilikuwa namaanisha nini , ” alisema Mbangu
kwa kujiamini .
TUREJEE NYUMA
Juni 25 , 2004, Babu Seya , Papii Kocha ,
Nguza Mbangu na Francis Nguza
walihukumiwa kifungo cha maisha jela
baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji
na kuwanajisi watoto 8 wa Shule ya Msingi ,
Mashujaa , Sinza jijini Dar. Hukumu hiyo
ilitolewa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi ya Kisutu chini ya Hakimu Eddy
Lyamuya. Walikata rufaa Mahakama Kuu .
Januari 27 , 2005 rufaa yao ya kwanza
ilisikilizwa ambapo Jaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo
aliitupilia mbali .
Februari 10 , 2010 Mahakama ya Rufaa
ilikazia hukumu ya Kisutu kwa Babu Seya na
Papii Kocha , lakini ikawaachia huru watoto
wengine wawili wa mwanamuziki huyo , Nguza
Mbangu na Francis Nguza .
Mwaka 2013 Babu Seya, Papii Kocha kupitia
kwa wakili wao Mabere Marando
waliwasilisha maombi ya kupitiwa upya kwa
rufaa ya hukumu yao, lakini jopo la majaji
watatu , Nathanieli Kimaro, Salum Masatu
na Mbaruk Salim walikazia hukumu ya
mwanzo baada ya hoja za serikali kuzizidi
zile za upande wa utetezi .

No comments:

Post a Comment

.