HII ni aibu kubwa! Mhadhiri wa Chuo cha
Kodi ya Mapato Tanzania, Richard Donati
amezuliwa timbwili la aina yake nyumbani
kwake, hali iliyosababisha mtaa kufungwa ,
kisa kikielezwa ni kukutwa na mchumba wa
mtu aliyetajwa kwa jina moja la Aisha .
Mwenye mchumba ( kushoto ) akitulizwa
baada ya kupandisha hasira .
HABARI KAMILI
Sakata hilo lilitokea mchana kweupe ,
Ijumaa iliyopita , Sinza – Kwa Remmy jijini
Dar es Salaam ambapo timu ya mapaparazi
wetu ilishuhudia mchezo mzima baada ya
kupigiwa simu na mmoja wa mashuhuda
walioona dalili za vurugu tangu mapema .
Shuhuda: “ Jamani hapo si OFM ( Oparesheni
Fichua Maovu)?”
OFM: “Ndiyo penyewe ndugu, tuambie. ”
Mhadhiri wa Chuo cha Kodi ya Mapato
Tanzania, Richard Donati (wa kwanza
kushoto ) baada ya tukio hilo.
Shuhuda: “ Kuna jamaa yuko hapa mtaani
kwetu Sinza- Kwa Remmy, amemfuata demu
wake kwa mshkaji mmoja hivi, ni ticha wa
Chuo cha Kodi ya Mapato Tanzania, njooni
haraka maana anamsubiri jamaa amtoe
ndiyo amchukue demu wake . Yupo hapa
getini, ” alisema shuhuda huyo .
KUMBE NI MWANAFUNZI WAKE!
Ndani ya dakika 15 , OFM wakawa wamefika
eneo la tukio na kukutana uso kwa uso na
aliyedai ni mwenye mali ambaye
alijitambulisha kwa jina moja la Ibra .
Alisema alikuwa eneo la tukio kwa ajili ya
kumchukua mchumba wake ambaye
anatembea na mwalimu wake huyo .
Wananchi wakilizonga gari alilokuwemo
mchumba wa mtu.
“Tangu asubuhi ameingia humu ndani , simu
amezima ili nisimpate. Ndugu zangu
naonewa, mimi nimetoka mbali na mchumba
wangu, nimeshaanza baadhi ya taratibu
nyumbani kwao . Najulikana kila mahali ,
naye anajulikana kwetu , lengo langu ni
kumuoa , lakini jamaa anaamua kutumia
ualimu wake kumdanganya mchumba wangu.
“Mimi najua anatumia mwanya wa kuwa
mwalimu wake ili kumfaidi . Mchumba wangu
anaogopa kumkataa kwa sababu anaweza
kumfelisha chuoni , naijua sana hiyo
michongo, ” alisema Ibra ambaye alikuwa
akizungumza kwa hisia kali, wakati
mwingine machozi yakimtoka.
Mchumba wa mtu akizidi kutulizwa na rafiki
yake.
MWENYE MALI, TICHA WAZOZANA
Ibra akiwa ameambatana na mjumbe wa
shina aliyetajwa kwa jina la mama Kibibi
na wapambe wengine waliokuwa eneo la
tukio, walifika getini kwenye nyumba ya
mwalimu huyo na kugonga , lakini kabla
mlango haujafunguliwa , gari aina ya
Toyota Harrier lilifika getini hapo na
dereva akapiga honi , geti likafunguliwa ,
gari likaingia ndani .
Muda mfupi baadaye mwalimu huyo alitoka
ndani na kuhoji uhalali wa Ibra kwenda
nyumbani kwake huku akidai hana
mamlaka ya kumfuata kwa kuwa msichana
yule ni mchumba tu na si mke .
Wananchi wakiwa eneo hilo la timwili .
Majibizano yalichukua nafasi kubwa kabla
ya Donati kukimbia ndani na kwenda
kujigonga kwenye ukuta jambo
lililosababisha apasuke usoni na kuanza
kuvuja damu .
Tukio hilo lilionekana kumchanganya sana
Donati na muda mfupi baadaye alitoka
mbio na kuelekea kusikojulikana.
IBRA , AISHA USO KWA USO
Aisha aliyekuwa ndani ya gari akiwa
amekaa siti ya dereva ( alihama kutoka siti
ya nyuma ) alipata nafasi ya kuzungumza
na Ibra ambaye alimsihi ashuke ili waende
nyumbani kwa wazazi wa binti huyo
kutafuta suluhisho .
Hata hivyo , msichana huyo alisikika
akisema: “ Ibra siwezi kushuka hapa. Aibu
yote hii ? Watu wamejaa hivyo , nitashukaje ?
Sishuki kwa kweli . ”
WANANCHI WAJA JUU
Umati uliokuwa eneo la tukio ulikuja juu
ukimtaka rafiki wa mwalimu Donati ( yule
aliyefika na Harrier) amfungulie mlango
Aisha ili aondoke na Ibra jambo ambalo
halikuzaa matunda hata kidogo .
Hata hivyo , kuna wakati jamaa huyo
alimwita Ibra pembeni na kuzungumza naye
wawili matatu na kisha Ibra kuamua
kuondoka zake.
IBRA NYUMA YA NONDO
Habari zilizopatikana wakati Wikienda
linakwenda mitamboni zinaeleza kuwa, Ibra
alikamatwa na askari na kufikishwa katika
Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini ’, Dar.
Inadaiwa alikamatiwa nyumbani kwa akina
Aisha ( hakukutajwa jina ) ambapo
alikwenda kwa lengo la kusuluhishwa na
wazazi wa binti huyo .
Monday, March 3, 2014
AIBU TICHA WA TRA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment