TUNAOMBA RADHI KWA
PICHA HII
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi
wa habari wa gazeti la American alinukuliwa
akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka
duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo
kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya
Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila
mafundisho yale yalikuwa mepesi sana
ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha.
Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata
zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The
Bettle). Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na
kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya
Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.
2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Alisema kwamba endapo angepata kura laki
tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil
na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza
kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa,
akapata kura zaidi ya hizo, akashinda
uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa,
akafariki dunia.
3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)
Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la
Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza
kuivuta, akachukua nyingine na kisha
kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako,
chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa
kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana
mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.
4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.
Baada ya kutengeneza meli ya Titanic,
mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani
ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana,
haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi
kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.
5. BON SCOTT (MUIMBAJI)
Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70
alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye
maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way,
down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa
amekufa baada ya kupaliwa na matapishi
yake.
6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana
kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake.
Wakati wanataka kuondoka na gari,
akamshika mtoto wake mkono garini na
kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie
katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari
imejaa mama, huyo Mungu labda akae
kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile
lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi
hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa.
Lilikuwa limebondeka sana na watu wote
walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza
polisi, trey la mayai wala halikuonekana
kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa
limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka
kutokutambulika.
7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA
HABARI)
Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma
vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu
kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo,
mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto
ambao haikujulikana mpaka leo ule moto
ulisababishwa na nini.
8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)Huyu
alifuatwa na Bill Graham na kumwambia
kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa
ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani,
akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema
"Simhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka
nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa
katika makazi yake. Polisi walijaribu
kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo
hawajapata jibu.
Kwa wale wanaotaka kujua mengi, wafungue
GOOGLE na kisha kusearch haya "People who
mocked GOD and died" Utasoma mengi tu.
Sunday, March 2, 2014
KUTANA NA WATU MAARUFU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUKUTWA NA MASWAHIBU MAKUBWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment