MASKINI! Stori zilizozagaa mitaani kuhusu
mali za aliyekuwa mkali wa sinema za
Kibongo, marehemu Steven Kanumba
zinasema kuwa , zimeuzwa na kampuni
aliyoiacha, Kanumba The Great Film
imefilisika, Ijumaa Wikienda linakupa
ripoti iliyoshiba .
Marehemu Steven Kanumba .
Habari zinadai kuwa baada ya kifo cha
Kanumba Aprili 7 , 2012, mali alizoziacha
zinafujwa, hakuna utaratibu mzuri wa
kusimamia mamb
na kwamba , uzalishaji wa sinema katika
kampuni yake ni mdogo tofauti na enzi za
uhai wake .
Chanzo chetu cha habari ambacho ni mmoja
wa wasanii wa filamu Bongo aliye na
ukaribu na familia hiyo , alisema ni kweli
kuna tatizo la usimamizi na uendelezaji wa
mali za marehemu lakini akasema ni jambo
la kawaida kwa sababu marehemu
ameondoka na mbinu zake.
Ofisi ya Kanumba ya Sinza Mori, Dar.
“Kila mtu ana nyota yake kaka,
asikudanganye mtu, lakini pia kila mmoja
ana namna anavyojua kuendesha biashara
zake, sasa Kanumba alikuwa na mikakati
yake, hawa walioachiwa nao wana mikakati
yao. Mfano , hawataweza kutoa sinema
nyingi kwa sababu soko la waliobaki si kubwa
kama ilivyokuwa kwa Kanumba .
“Angalia hata ushindani. .. hivi kweli Seth
(Bosco , ‘ mdogo wa Kanumba ’) anaweza
kupambana na magwiji kama JB ( Jacob
Steven ) au Ray (Vincent Kigosi) sokoni ?
Watu waache lawama, ” alisema msanii huyo
ambaye aliomba hifadhi ya jina .
Marehemu Kanumba enzi za uhai wake
akiwa pembeni ya gari lake .
MDOGO WAKE ABANWA
Waandishi wa habari hizi walifunga safari
hadi Sinza –Mori, Dar zilipo Ofisi za
Kanumba The Great Film na kuzungumza na
mdogo wa marehemu Kanumba , Seth Bosco
ambaye alisisitiza kampuni ya marehemu
kaka yake haijafilisika kama maneno
yalivyozagaa mitaani.
“Hao wanaosema eti kampuni ya Kanumba
imefilisika wanakurupuka tu, hawana cha
kufanya lakini nataka kuwahakikishia
kuwa, hatujayumba ila tunakabiliwa na
changamoto za kawaida tu kama
inavyokuwa kwa kampuni nyingine, ” alisema
Seth.
Toyota Hiace aliyokuwa anamiliki Kanumba .
HIACE, TOYOTA GX 110
WIKIENDA : Lakini Seth kuna maneno kuwa
lile gari aina ya Toyota GX 110 na Toyota
Hiace lilikokuwa likitumika kwenye kurekodi
sinema yameuzwa , ni kweli ?
SETH: Ni kweli Hiace tumeiuza lakini
tumenunua Noah kwa kazi hiyohiyo ya
‘location ’, kuhusu GX 110 halijauzwa , lipo
nyumbani hata sasa hivi ukienda utalikuta .
KUHUSU LEXUS
WIKIENDA : Tulisikia gari alilokuwa
akitembelea marehemu Kanumba , Toyota
Lexus limeuzwa. Ni kwa nini na liliuzwa kwa
bei gani?
SETH: Kama familia tuliamua kuliuza kwa
sababu ya gharama za uendeshaji . Lile gari
linatumia mafuta mengi sana na
matengenezo yake ni makubwa na
hatukuona sababu za kuingia kwenye
gharama kubwa za namna hiyo .
Kuhusu bei lililouziwa, kwa kweli sifahamu.
Kama unavyojua baada ya mtu kufariki
dunia, huwa kuna msimamizi wa mirathi ,
yeye ndiye anayejua kuhusu hilo .
Mama mzazi wa Kanumba , Flora Mtegoa .
UZALISHAJI
WIKIENDA : Kipindi cha Kanumba , alikuwa
akitoa sinema nyingi sana , nadhani kama
sikosei ilikuwa moja kila baada ya miezi
miwili wakati mwingine kila mwezi sinema
moja lakini baada ya yeye kuondoka ,
uzalishaji hakuna tena .
Mfano mpaka sasa kuna sinema mbili tu
sokoni tangu alipokufa ambapo inakaribia
miaka miwili sasa. Tatizo ni nini?
SETH: Ni kweli , lakini si kwa sababu ya
tatizo la fedha – ni uhitaji . Unajua kuna
changamoto nyingi sana kwenye tasnia yetu .
Ni kweli mpaka sasa tumetoa sinema mbili;
Malaika na Wonderful Girl ambayo tayari
iko kwa msambazaji lakini bado haijaingia
mitaani.
Mwaka huu ndiyo tumeanza, kuna kazi
moja tunaifanya sasa hivi, ingawa si ya
kwetu, sisi tunasimamia kwenye production
(kuizalisha ) lakini mipango ya mwaka huu
ni mikubwa , mapema sana , tutaanza
kurekodi kazi yetu nyingine , kwa sasa siwezi
kusema jina lake ila inakuja .
Mdogo wa marehemu Kanumba , Seth Bosco.
OFISI VIPI ?
WIKIENDA : Kwa nini muda mwingi ofisi
inakuwa imefungwa tofauti na ilivyokuwa
kwa marehemu Kanumba ?
SETH: Kaka hii ni kampuni , sisi tunafanya
biashara na mteja wangu hahitaji
kunifuata . Mimi mteja wangu ni Steps ,
ambaye namtayarishia kazi kisha
nampelekea.
Milango inaweza kuwa imefungwa lakini
kazi za ‘editing ’ zikawa zinaendelea ndani
au tukafunga ofisi lakini tukawa location
tunarekodi, kuna tatizo gani hapo ?
WIKIENDA : Lakini marehemu alikuwa
anauza hadi filamu hapa ofisini ?
Imekuwaje siku hizi?
SETH: Hatujawahi kuuza sinema hapa ofisini
ila tulikuwa tunaweka kama mfano wa kazi
zilizowahi kufanywa na marehemu – si za
watu wala kampuni nyingine . Lengo lilikuwa
kuwapa watu wanaotutembelea ( bure) , si
kwa kuwauzia .
Bila shaka maelezo hayo ya Seth yatakuwa
yamejibu maneno yote yanayosemwa
mitaani.
Monday, March 3, 2014
RIPOTI KAMILI
AIBU TICHA WA TRA
HII ni aibu kubwa! Mhadhiri wa Chuo cha
Kodi ya Mapato Tanzania, Richard Donati
amezuliwa timbwili la aina yake nyumbani
kwake, hali iliyosababisha mtaa kufungwa ,
kisa kikielezwa ni kukutwa na mchumba wa
mtu aliyetajwa kwa jina moja la Aisha .
Mwenye mchumba ( kushoto ) akitulizwa
baada ya kupandisha hasira .
HABARI KAMILI
Sakata hilo lilitokea mchana kweupe ,
Ijumaa iliyopita , Sinza – Kwa Remmy jijini
Dar es Salaam ambapo timu ya mapaparazi
wetu ilishuhudia mchezo mzima baada ya
kupigiwa simu na mmoja wa mashuhuda
walioona dalili za vurugu tangu mapema .
Shuhuda: “ Jamani hapo si OFM ( Oparesheni
Fichua Maovu)?”
OFM: “Ndiyo penyewe ndugu, tuambie. ”
Mhadhiri wa Chuo cha Kodi ya Mapato
Tanzania, Richard Donati (wa kwanza
kushoto ) baada ya tukio hilo.
Shuhuda: “ Kuna jamaa yuko hapa mtaani
kwetu Sinza- Kwa Remmy, amemfuata demu
wake kwa mshkaji mmoja hivi, ni ticha wa
Chuo cha Kodi ya Mapato Tanzania, njooni
haraka maana anamsubiri jamaa amtoe
ndiyo amchukue demu wake . Yupo hapa
getini, ” alisema shuhuda huyo .
KUMBE NI MWANAFUNZI WAKE!
Ndani ya dakika 15 , OFM wakawa wamefika
eneo la tukio na kukutana uso kwa uso na
aliyedai ni mwenye mali ambaye
alijitambulisha kwa jina moja la Ibra .
Alisema alikuwa eneo la tukio kwa ajili ya
kumchukua mchumba wake ambaye
anatembea na mwalimu wake huyo .
Wananchi wakilizonga gari alilokuwemo
mchumba wa mtu.
“Tangu asubuhi ameingia humu ndani , simu
amezima ili nisimpate. Ndugu zangu
naonewa, mimi nimetoka mbali na mchumba
wangu, nimeshaanza baadhi ya taratibu
nyumbani kwao . Najulikana kila mahali ,
naye anajulikana kwetu , lengo langu ni
kumuoa , lakini jamaa anaamua kutumia
ualimu wake kumdanganya mchumba wangu.
“Mimi najua anatumia mwanya wa kuwa
mwalimu wake ili kumfaidi . Mchumba wangu
anaogopa kumkataa kwa sababu anaweza
kumfelisha chuoni , naijua sana hiyo
michongo, ” alisema Ibra ambaye alikuwa
akizungumza kwa hisia kali, wakati
mwingine machozi yakimtoka.
Mchumba wa mtu akizidi kutulizwa na rafiki
yake.
MWENYE MALI, TICHA WAZOZANA
Ibra akiwa ameambatana na mjumbe wa
shina aliyetajwa kwa jina la mama Kibibi
na wapambe wengine waliokuwa eneo la
tukio, walifika getini kwenye nyumba ya
mwalimu huyo na kugonga , lakini kabla
mlango haujafunguliwa , gari aina ya
Toyota Harrier lilifika getini hapo na
dereva akapiga honi , geti likafunguliwa ,
gari likaingia ndani .
Muda mfupi baadaye mwalimu huyo alitoka
ndani na kuhoji uhalali wa Ibra kwenda
nyumbani kwake huku akidai hana
mamlaka ya kumfuata kwa kuwa msichana
yule ni mchumba tu na si mke .
Wananchi wakiwa eneo hilo la timwili .
Majibizano yalichukua nafasi kubwa kabla
ya Donati kukimbia ndani na kwenda
kujigonga kwenye ukuta jambo
lililosababisha apasuke usoni na kuanza
kuvuja damu .
Tukio hilo lilionekana kumchanganya sana
Donati na muda mfupi baadaye alitoka
mbio na kuelekea kusikojulikana.
IBRA , AISHA USO KWA USO
Aisha aliyekuwa ndani ya gari akiwa
amekaa siti ya dereva ( alihama kutoka siti
ya nyuma ) alipata nafasi ya kuzungumza
na Ibra ambaye alimsihi ashuke ili waende
nyumbani kwa wazazi wa binti huyo
kutafuta suluhisho .
Hata hivyo , msichana huyo alisikika
akisema: “ Ibra siwezi kushuka hapa. Aibu
yote hii ? Watu wamejaa hivyo , nitashukaje ?
Sishuki kwa kweli . ”
WANANCHI WAJA JUU
Umati uliokuwa eneo la tukio ulikuja juu
ukimtaka rafiki wa mwalimu Donati ( yule
aliyefika na Harrier) amfungulie mlango
Aisha ili aondoke na Ibra jambo ambalo
halikuzaa matunda hata kidogo .
Hata hivyo , kuna wakati jamaa huyo
alimwita Ibra pembeni na kuzungumza naye
wawili matatu na kisha Ibra kuamua
kuondoka zake.
IBRA NYUMA YA NONDO
Habari zilizopatikana wakati Wikienda
linakwenda mitamboni zinaeleza kuwa, Ibra
alikamatwa na askari na kufikishwa katika
Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini ’, Dar.
Inadaiwa alikamatiwa nyumbani kwa akina
Aisha ( hakukutajwa jina ) ambapo
alikwenda kwa lengo la kusuluhishwa na
wazazi wa binti huyo .
WASTARA ASUMBULIWA NA ROHO YA KIFO
Stori : Gladness Mallya na Hamida Hassan
OOOH! Zikiwa zimepita siku chache tangu
staa wa filamu Bongo , Wastara Juma
kunusurika kifo baada ya kudaiwa kunywa
sumu na baadaye kupata ajali , anadaiwa
kusumbuliwa na roho wa kifo .
Wastara Juma .
Kupitia ukurasa wake katika Mtandao wa
Kijamii wa Instagram, Wastara aliweka
picha za wasanii mbalimbali huku
akimwelezea kila mmoja alivyo na mwishoni
mwa maelezo hayo alimalizia kwa kusema
kuwa ameamua kusema kabla hajafa kwani
kifo hakiko mbali .
00Baadhi ya mastaa aliowaelezea ni
Tamrina Poshi ‘ Amanda’, Denis Swea ‘Dino ’ ,
Jacob Steven ‘JB ’, Steven Mengere ‘ Steve
Nyerere ’, Halima Yahya ‘ Davina’, Riyama
Ally, Salma Jabu ‘ Nisha’.
Wengine ni Cloud , Lamata , Bondi , Msafiri
Kondo na wengineo ambapo baada ya
kumuelezea kila mmoja , chini alikuwa
akiandika ujumbe huu:
“Sababu ya kufanya hivi, sisi ni binadamu
na kifo hakiko mbali , naweza nikafa kabla
sijasema lolote kwa watu wangu .”
WASTARA ANASEMAJE ?
“Niliandika maneno hayo ili wasanii wote
waliowahi kunitendea wema wajue kwamba
wao ni watu muhimu sana katika maisha
yangu , wapo wengi lakini sikuweza
kuwashukuru wote kwa sababu wakati
naandika hivyo nilikuwa kwenye hali mbaya
sana.
“Unajua siku moja nitakufa maana kifo
kiko karibu sana hivyo watakumbuka
maneno yangu hayo niliyoandika ya
kuwashukuru, ” alisema Wastara .
Baada ya kuwaelezea kwa kuwaandikia
waraka huo, mashabiki mbalimbali waliopo
kwenye mtandao huo walionekana
kusikitishwa na maneno hayo na kujikuta
wakimuuliza maswali yasiyokuwa na majibu
kwa wakati huo huku wengine wakidai kuwa
Wastara anasumbuliwa na roho wa kifo .
MLELA: ULEZI UMENIFICHA
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu,
staa wa filamu Bongo , Yusuf Mlela
amefunguka kuwa ukimya huo
umesababishwa na malezi ya mwanaye.
Yusuf Mlela.
Akichonga na gazeti hili , Mlela alisema
anahitaji muda mwingi kukaa na mwanaye
Mwantumu kama baba hivyo majukumu
yamekuwa mengi , anawaomba mashabiki
wake kuelewa kwani ‘soon’ atakuja
kivingine .
“Muda mwingi nautumia kukaa na
mwanangu hata yale mambo ya kuzunguka
hovyo kwenye starehe hakuna tena ila
pamoja na malezi bado najiiba kuandaa
kazi zangu za filamu na muda siyo mrefu
nitaanza kuzitoa , ” alisema Mlela .
NISHA AWA KITUKO KWA YATIMA
STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘ Nisha’
hivi karibuni alijikuta akigeuka kituko kwa
watoto yatima kutokana na mavazi ya
‘kihasara ’ aliyokuwa amevaa na kulazimika
kujistiri na mtandio kiunoni .
Salma Jabu ‘Nisha’ .
Nisha akiwa na timu yake (Team Nisha),
walikwenda kutoa msaada katika Kituo cha
Mwana Orphans Centre kilichopo Vingunguti ,
jijini Dar na walipofika walijishangaa kwa
kuwa watoto hao walikuwa wamevaa mavazi
ya heshima .
“Mh ! Imebidi nijistiri kidogo na mtandio
lakini kimsingi nimeguswa na watoto hawa
kwa sababu na mimi ni yatima na haya
maisha nimeyapitia hivyo kila mwisho wa
mwezi tutakuwa tukitembelea kituo hiki na
kuwaletea mahitaji muhimu , ” alisema Nisha.
Nisha na wenzake walitoa misaada ya vifaa
mbalimbali vikiwemo sabuni, vyakula na
vinywaji huku mmoja wao aliyekuwa na
‘bethdei ’ akikata keki na kula na watoto
hao.
Load Previous Comments
SHAMSA: MSIMSOGELEE MUME WANGU!
MWADADADA anayefanya poa Bongo Movies ,
Shamsa Ford amewataka wanawake
wanaomfuatilia mumewe, Dickson waache
mara moja .
Shamsa Ford .
Shamsa alisema, anakerwa sana na tabia ya
wanawake wanaomfuata mumewe kwani
hata wale wa ‘zilipendwa ’ wameanza
kujirudisha upya kitu ambacho
hatakubaliana nacho.
“Hawa wanawake hawana adabu wala aibu ,
ninawatahadharisha tu, wakae mbali na
mume wangu kabla sijawaanika hadharani
kwenye vyombo vya habari , kwanza
hawawezi kufanikiwa , najiamini, ” alisema
Shamsa.
REHEMA FABIAN LAIVU
KhAA! Mshiriki wa Shindano la Miss Kiswahili
mwaka 2009 ambaye kwa sasa yuko nchini
China akijitafutia maisha, Rehema Fabian
amenaswa laivu akiwa kimahaba na kibabu
cha kizungu .
Miss Kiswahili mwaka 2009, Rehema Fabian ,
akiwa kimahaba na kibabu cha kizungu .
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia
ya simu , mnyetishaji wetu ambaye naye
yuko nchini humo alisema kuwa kwa sasa
mrembo huyo anajiachia na babu huyo
ambaye kwa kumwangalia harakaharaka
anaweza kuwa sawa na mjukuu wake .
Rehema Fabian .
“Unajua mapenzi ya wazee ni mazuri sana ,
kwanza wanajua kubembeleza , isitoshe
hawakupi msongo wa mawazo mara kwa
mara kama yalivyo mapenzi ya vijana na
ndiyo maana Rehema akaona bora ajiachie
na kibabu , ” alisema mtonyaji huyo .
Rehema Fabian .
Baada ya kupata ‘ infomesheni ’ hizo ,
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Rehema ili
kujiridhisha kuhusiana na stori hiyo ambapo
kwa upande wake alianza kucheka kisha
kudai aachwe ale ujana.
“Ahaha! Mshaanza mambo yenu , niacheni
jamani nile ujana, ” alisema Rehema .