BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu
maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh
50,000.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema
jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa
madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa
kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa
katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia
malipo ya aina yoyote.
Sarafu hii imetolewa maalumu kama
maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya
Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana
na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya
BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu
hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa
ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi
kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu
hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa
Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo
kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu
ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na
kimataifa.
“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya
sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida
zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa
Ndulu.
Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana
Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi
ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata
sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu,
Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko
Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza
sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema
gavana na kuongeza taarifa za usambazaji
zitatolewa na benki hizo.
Katika sarafu hiyo, upande wa mbele
unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman
Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa
Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi’.
Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo
ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi
yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”,
thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.
-Tanzania daima
Friday, January 3, 2014
HOT NEWZZ BANK KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YA SH 50,000/-
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hapo nimewaelewa. ila ingekua inaingwi ktk mfumo wa malipo
ReplyDeleteKudadeki
ReplyDeleteNOMA SANA
ReplyDeletehehehehe...itakuwa balaaaaaa
ReplyDeletesijawaele lengo kuu nn hata kama maadhimisho inafaida gan na kwa nan natamn gavana aje hapa nimuulze yaliypo myon
ReplyDelete