.
KATIKA staili ya aina yake ya kuuaga mwaka
na kuukaribisha 2014, mtangazaji Peniela
Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa
Nasib Abdul ‘Diamond’ alipewa zawadi
ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii
nyumbani kwake Mwananyamala Mwinjuma
alikohamia hivi karibuni, baada ya watu
wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema
Sepetu, kufika hapo wakiwa na ‘mzigo’ huo
uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua.
Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi
Penny, aliliambia gazeti hili kuwa msafara
wa magari matatu ulifika hapo na kugonga
mlango wakimuulizia mtangazaji huyo wa
kituo cha televisheni cha Channel Ten.
“Walivyofika sisi tulijua labda leo ni bethidei
ya Penny, maana tuliwaona wakiwa na maua,
keki, shampeni na kadi, walipomuulizia
tukawaambia ametoka, wakaacha mzigo huo
wakisema apewe atakaporudi,” alisema
shuhuda huyo.
Juu ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji
huyo kulikuwa na maandishi yaliyomsuta na
kumtaka kuachana na tabia ya kuchukua
mabwana wa rafiki zake pamoja na dada
zake, hali inayoonyesha kuwa waliompelekea
ujumbe huo ni wabaya wake.
Juhudi za kumtafuta Penny kuzungumzia
tukio hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi
gazeti hili linakwenda mtamboni
Friday, January 3, 2014
PICHAZ..MASKINI PENNY "ZILIPENDWA WA DIAMOND" ABWAGIWA KEKI YA KUSUTWA NA MANENO MAKALI..ICHEKI HAPA..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hahahahahaaa kudadadadekiii
ReplyDelete