MSANII wa filamu, Rose Ndauka amejifungua
mtoto wa kike Jumapili iliyopita katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na
kusisitiza, amefanana na baba yake.
Ndauka ambaye miezi michache iliyopita,
alitangaza kusimama kuigiza kwa muda wa
mwaka mmoja ili ajitathmini alijifungua mtoto
huyo kwa operesheni.
Katika mazungumzo na Mwanaspoti, Ndauka
alisema: “Namshukuru Mungu, nimefanikiwa
kujifungua salama, mtoto mwanamke.”
“Ni faraja kwangu kwa sababu nimepata
mwenzangu na amefanana na baba yake mzazi
(Pichani),” alisema Ndauka bila kutaja jina la
baba wa mtoto huyo.
Ndauka ni mwigizaji maarufu wa filamu
anayekubalika katika tasnia hiyo huku
akitamba na kazi zake mbalimbali zikiwamo,
Bad Girl, Fall in Love na nyinginezo.
Friday, January 3, 2014
ROSE NDAUKA AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hongera yake
ReplyDelete