Timu ya Yanga Fc .
Na Sweetbert Lukonge
TIMU ya Yanga huenda isialikwe tena
katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi
ambayo hufanyika kila mwaka kisiwani
Zanzibar, kutokana na tabia yake ya
kujitoa katika dakika za mwisho .
Kamati ya Maandalizi ya Kombe la
Mapinduzi imeamua kuishtaki Yanga kwa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inayoongozwa na Rais wa Dkt Ali Mohamed
Shein, ambayo ndiyo waratibu wakuu wa
mashindano hayo.
Msemaji wa kamati hiyo , Farouq Karim
ameliambia gazeti hili kuwa walijitahidi
kuhakikisha Yanga inashiriki mashindano
hayo lakini kitendo hicho cha kujiondoa
dakika za mwisho kimevuruga uhusiano
mzuri uliokuwepo baina ya klabu hiyo na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Alisema kwa miaka mingi Yanga imekuwa
ikialikwa kushiriki mashindano hayo lakini
imekuwa ikionyesha tabia mbaya kwa
Serikali ya Zanzibar ambayo rais wake wa
kwanza , Sheikh Amri Abeid Karume alikuwa
ni miongoni mwa waasisi wa klabu hiyo
kongwe kabisa hapa nchini.
“Yanga ndiyo timu pekee ya Tanzania
ambayo ilitakiwa iwe inayaheshimu
mashindano haya kuliko klabu nyingine zote
kutokana na historia nzuri iliyonayo na
Serikali ya Zanzibar.
“Tumeamua kuishitaki kwa serikali na
ikiwezekana kuanzia sasa isiitwe tena
kushiriki mashindano haya , ” alisema Karim .
Friday, January 3, 2014
Yanga yashitakiwa kwa rais wa Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment