Friday, January 3, 2014

KIFO CHA WAZIRI MGIMWA , KWA NINI ..


Na Mwandishi Wetu
WAKATI taifa likiwa katika msiba kufuatia
kifo cha Waziri wa Fedha, Mipango na
Uchumi, Dk. William Mgimwa , wananchi
wameitaka serikali kueleza kwa nini kwa
kipindi chote cha kuumwa kwake, ugonjwa
uliomuua ulifanywa siri .
Marehemu Dk . William Mgimwa .
Waziri Mgimwa alifariki dunia Jumatano
(juzi ) saa 5 : 20 asubuhi kwa saa za Afrika
Kusini ( Tanzania saa 6 : 20 ) katika Hospitali
ya Mediclinic Klooff jijini Johannesburg
nchini humo.
Vyanzo mbalimbali kutoka wizara hiyo
vinasema , waziri Mgimwa ambaye pia ni
mbunge wa Jimbo la Kalenga , Iringa, kabla
ya kuugua alikuwa na wakati mgumu
kiutendaji kutokana na shinikizo
mbalimbali alizokuwa akizipata.
“Kuna mambo sana pale wizarani , waziri
alikuwa na wakati mgumu sana , haya
mambo ndiyo yalimfanya hata akajikuta
anapata matatizo na kuugua , ” kilisema
chanzo hicho ambacho kilikataa kutoa
ufafanuzi zaidi wa mambo hayo
yaliyomtokea kiongozi huyo .
Ijumaa liliwasiliana na daktari mmoja
bingwa wa magonjwa ya binadamu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH ) na
kuulizwa kama mtu ambaye ana matatizo
ya mara kwa mara kazini kwake na
kufokewa au kupewa amri anaweza kupata
na tatizo gani, akafafanua .
Akifafanua zaidi , daktari huyo kwa sharti
la kutotajwa jina lake gazetini alisema upo
uwezekano wa marehemu Mgimwa kuwa
alipata ugonjwa unaosababishwa na damu
kuganda na kuziba kwenye njia ya mishipa .
“Kama mnasema alikuwa akipata shinikizo
huko kazini kwake, basi huenda alitokewa
na kitu kinachoitwa kitaalam Trans
Ischaemic Attack ( TIA) . Hii ni hali ya damu
au mafuta kuganda na kuziba kwenye
mishipa, hivyo kusababisha damu kushindwa
kutembea kuelekea sehemu mbalimbali
kwenye mfumo wa ubongo , ” alisema daktari
huyo na kuongeza:
“Mara nyingi watu wanaopata tatizo hilo
husababishwa na kupewa taarifa za kushtua
kama kufokewa au kugombeshwa na
kusababisha msongo wa mawazo.”
Akitoa ufafanuzi zaidi , daktari huyo
alisema, TIA huweza kumtokea mtu yeyote
na kwamba kwa kawaida, hudumu kati ya
dakika moja hadi tano na anayekutwa na
hali hiyo , kama asipopatiwa tiba mapema ,
huwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa
kupooza ( stroke).
“Lakini kama hali hiyo itaendelea kuwepo
pasipo damu au mafuta yaliyoganda
kuyeyuka, basi mishipa hushindwa kupitisha
damu kuelekea sehemu za ubongo na hivyo
kusababisha eneo hilo kufa. Kadiri TIA
inavyokaa muda mrefu ndivyo madhara
yanavyokuwa makubwa ya kuweza
kusababisha kupooza au hata kifo , ”
alisema.
Hata hivyo , wananchi wameishauri serikali
kuweka wazi taarifa za maradhi ya viongozi
wa ngazi za kitaifa ili kuondoa
sintofahamu mitaani.

No comments:

Post a Comment

.