Friday, February 28, 2014

MSAIDIE MTOTO HUYU AWEZE KUTIBIWA

MTOTO Adolotea Njavike( 1 . 4 ) anaomba
msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria
wema ili aweze kufanyiwa upasuaji
kutokana na kichwa na kiwiliwili kuungana
baada ya kupata ajali ya moto akiwa na
mama yake mzazi.
Akizungumza kwa masikitiko, mama mkubwa
wa mtoto huyo , Salome Kiegu ( 35 ) mkazi wa
mtaa wa Maendeleo Iyunga jijini Mbeya
anasema mtoto huyo akiwa na mama yake
walipata janga la moto katika mazingira ya
kutatanisha walipoangukia kwenye moto
ambapo mtoto huyo aliungua vibaya.
Anasema tukio hilo lilitokea Agosti mwaka
jana lakini alipopatiwa matibabu katika
kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi
ya kidevu na kifua hali inayomletea shida
wakati wa kula na kushindwa kufurahi na
wenzake .
Anasema tangu kipindi hicho alimchukua
mtoto huyo kwa mama yake na kuanza
kuomba msaada wa matibabu baada ya
kumpeleka Hospitali ya Ikonda iliyoko
Makete Mkoani Njombe ambapo wataalamu
walimwambia atafute shilingi milioni moja
ili mtoto wake aweze kutibiwa .
Ameongeza kuwa baada ya muda
wataalamu hao walimwambia asubiri
Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza
kumtibia mwanaye ambapo baada ya
kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao
walifika na kumcheki mtoto kisha
kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa
aende CCBRT Dar Es Salaam ambako
ataweza kutatuliwa tatizo lake .
Aidha kutokana na maelezo hayo , Mama
huyo anaomba msaada kutoka kwa
wasamaria wema ili aweze kufanikisha
matibabu ya mtoto wake .
Amesema anahitaji zaidi ya shilingi milioni
mbili ili ziweze kumsaidia kusafiri ,
kugharamia matibabu pamoja na huduma
nyingine wakati akisubiri matibabu ya
mwanaye.
Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo
anaweza kuwasiliana moja kwa moja na
mama huyo kupitia simu yake ya mkononi
namba 0752 986879 au Nyumbani kwake
Iyunga, mtaa wa Maendeleo jijini Mbeya .

No comments:

Post a Comment

.