SKENDO nzito ya Bongo Muvi imeibuliwa na
baadhi ya wabunge waliopo mjini Dodoma
kufuatia kuwalipua wasanii wake kuwa, ni
ombaomba balaa , Risasi Jumamosi lina
mkanda mzima .
Kwa mujibu wa wabunge hao ambao walitaka
majina yao yasitiriwe kwa sasa, baadhi ya
wasanii hao ambao wengi ni mastaa
wamekuwa wakiwazukia na kuwapiga
mizinga jambo linalowashangaza hasa
wakizingatia kuwa , wapiga mizinga hao
wana majina makubwa na huonekana
wakitembelea magari ya kifahari .
Staa wa filamu za Kibongo , Jacqueline
Wolper .
“Hivi nyie mapaparazi , mnashindwa kabisa
kukomesha hii tabia ya mastaa wa Bongo
Muvi? Hawa jamaa ni ombaomba sana.
“Wamekuwa wakitupiga mizinga sana .
Tunawashangaa maana wengine wana
majina makubwa , wanatembelea magari ya
kifahari lakini bado wanaomba pesa
ndogo , ” alisema mbunge mmoja ambaye
anatoka kwenye moja ya majimbo ya Mkoa
wa Dar es Salaam.
KINACHOWASHANGAZA WABUNGE
Kwa mujibu wa wabunge hao ,
linalowashangaza zaidi ni kwamba wasanii
hao ambao ni wake kwa waume , wamekuwa
wakipiga mizinga ya pesa ndogo badala ya
kuomba pesa za kufanyia mambo makubwa
yenye mikakati mizito.
Steve Mangere ‘ Steve Nyerere ’.
“Mtu anakuja , anasema anasumbuliwa na
kodi ya nyumba au anasema hajala . Hivi
kweli mastaa wakubwa kama akina …
(anataja jina ) ni wa kuomba vijisenti kama
vya kodi ya nyumba jamani?” alihoji
mbunge mwingine kati ya watano waliokuwa
wakizungumza na gazeti hili .
Waheshimiwa hao waliendelea kuwaanika
mastaa hao kwa kudai kwamba ,
walichogundua ni kuwa inapotokea
wakapewa hitaji lao la fedha, huishia
kukaa baa hadi usiku wa manane na
asubuhi wakiamka wako vilevile kama
hawakupewa .
Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania ‘ TAFF ’ , Simon Mwakifwamba.
MWAKIFWAMBA ABANWA NA RISASI
Ili kuweka sawa madai hayo mazito na
yenye aibu kubwa kwa tasnia hiyo maarufu
nchini, Risasi Jumamosi lilimtafuta Rais wa
Shirikisho la Filamu Tanzania ‘ TAFF ’, Simon
Mwakifwamba ambaye alikiri kuwepo kwa
malalamiko hayo ya wasanii wake kuwa
ombaomba!
HUYU HAPA MWAKIFWAMBA
“Ni kweli kabisa. Mimi mwenyewe nimewahi
kusikia malalamiko hayo, lakini unajua
tena ni mambo binafsi, mtu anapiga
mizinga kwa mambo binafsi si rahisi
kumwingilia, ” alisema rais huyo .
Aliendelea kusema kuwa , katika vikao
mbalimbali vya kisanii , amewahi kuweka
wazi msimamo wa taasisi kwamba kila
msanii aishi maisha yenye heshima huku
akiwa mbali na mazingira yenye
kusababisha aibu katika jamii.
Rais wa Tanzania ,
Mheshimiwa Jakaya Kikwete ‘JK’ .
KUMBE HATA JK ALIWAHI KUMLALAMIKIA
Katika kuonesha hasira zake juu ya tuhuma
hizo zenye dharau katika gemu la filamu ,
Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa
kusema kuwa, katika moja ya mazungumzo
yake na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Kikwete ‘JK ’ aliwahi kumlalamikia
kwamba, wapo mastaa ambao kazi yao ni
kupiga mizinga isiyo na tija.
“Rais mwenyewe aliwahi kuniambia kuna
wasanii wakiwasiliana na yeye
wanamwambia mambo ya pesa za kula.
“Kuna msanii aliwahi kumtumia meseji JK
akimwambia, ‘mjukuu wako leo hali
mbaya’ , ” alisema Mwakifwamba.
Akaendelea : “ Sasa we’ unakutana na rais
badala ya kumweleza mikakati mikubwa na
nini cha kusaidiwa kuifanya tasnia iweze
kuendelea , unapiga mizinga hujala , ni aibu
sana. ”
Waziri Mkuu, Mh . Mizengo Pinda .
WALISHAMPIGA ‘MIZINGA ’ HADI ‘MTOTO WA
MKULIMA ’
Mwakifwamba hakukubali kufumba midomo
yake bila kupasua yote ambapo alizidi
kudai kuwa , hawashangai sana wasanii
wake hao kwani waliwahi kumpiga mizinga
hadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza
Peter Pinda ‘Mtoto wa Mkulima ’.
“Niliwahi kukutana na Waziri Mkuu Pinda,
nikamwomba mambo ya kuisaidia tasnia ya
filamu Tanzania , akasema afadhali mimi
nimeongea vitu vya maana, kuna wenzangu
alikutana nao ‘wakambomu ’ fedha za
matumizi binafsi, nilishangaa sana , ”
alisema Mwakifwamba.
RISASI LAWASAKA MASTAA, WAPATIKANA
HAWA:
Jacqueline Wolper , ni staa wa filamu za
Kibongo. Filamu yake ya kwanza ni Ama Zao
Ama Zangu. Yeye alipoulizwa kuhusu madai
hayo, alisema :
“Ni kweli , sikatai kwamba hiyo tabia ipo
tena sana tu . Lakini wanaoongoza ni
mastaa wa kiume , hao ndiyo wanaotutia
aibu ya kuonekana sisi ni o
mbaomba.”
STEVE NYERERE
Yeye ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity.
Alisema anavyojua kuna kuonana kirafiki
na waheshimiwa na kuonana kiajenda .
“Tabia ya kuomba fedha kwa waheshimiwa
ipo. Lakini linapokuja suala la tasnia yetu
kupeleka hoja kwao , tunaanza hoja baada
ya hapo kuna waheshimiwa wengi wana
urafiki na wasanii , tunaitana pembeni na
kupiga kirungu .
“Siwezi kukaa na waheshimiwa kama Rostam
Aziz , William Ngeleja, Mheshimiwa Abood na
Nimrod Mkono halafu nikawaacha hivihivi,
kisa eti mimi ni Mwenyekiti wa Bongo Muvi , ”
alisema Steve akionesha kumshangaa
mwandishi aliyempigia simu kutaka usawa
wa mizani ya habari hiyo .
Jennifer Kyaka ‘ Odama ’.
ODAMA YEYE
Jennifer Kyaka ‘Odama ’ yeye alipata
umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya
Odama iliyokuwa ikirushwa na Televisheni ya
Taifa ( wakati huo TVT ) . Alipopigiwa simu
iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha
ya kurudiwa mara kadhaa .
Aunt Ezekiel
AUNT EZEKIEL
Risasi pia lilimtafuta nyota mwingine aliye
mahiri kwenye sinema za Bongo, Aunt
Ezekiel ambaye filamu iliyompaisha sana
inaitwa Miss Tanzania. Yeye simu yake ya
mkononi ilionesha kutokuwa hata na laini
kwa wakati huo.
Staa mkongwe katika gemu , Vincent Kigosi
‘ Ray ’.
RAY AFUNGUKA
Staa mkongwe katika gemu tangu enzi za
Kaole Sanaa Group , Vincent Kigosi ‘ Ray ’
aliposakwa na kuulizwa kuhusu madai hayo
ya wasanii kuwa ombaomba alisema:
“Wasanii wengi wanawaza maisha ya hapa
na si baadaye . Badala ya mtu kuweka shida
zake kwenye mfuko wa karatasi , anaweka
kwenye rambo ambao unapiga kelele .
“Mwisho wa siku anaomba shilingi milioni
tatu akagombolee gari au asaidiwe kodi ya
nyumba , anasahau kuwa kapata nafasi ya
kuonana na mheshimiwa azungumzie tasnia
tunavyonyonywa hadi kuuza hati miliki, ”
alisem Ray .
Saturday, March 1, 2014
WABUNGE WAWALIPUA BONGO MOVIE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment