Tuesday, March 4, 2014

ABIRIA AJICHINJA NDANI YA BASI


Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
AMA kweli duniani kuna mambo kwani
dereva na abiria wa basi la Manchester
ambalo namba yake haikujulikana mara
moja , lililokua likitoka Lindi kwenda jijini
Dar es Salaam walijikuta wakiangua vilio
baada ya kumuona mwenzao akijichinja
hadi kufa kwa kisu ndani ya gari hilo .
Ujumbe kabla ya kifo : Kijana aliyejichinja
ndani ya basi akiandika ujumbe kabla ya
kukata roho.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la
kusikitisha lilitokea saa tisa alasiri,
Jumatano wiki iliyopita mara basi hilo
lilipofika katika hoteli moja ya Nangulukulu
kwa ajili ya kupatia chakula.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na
waandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya
abiria walioshuhudia tukio hilo walisema
kuwa mara walipofika katika hoteli hiyo ,
kila mmoja alitawanyika kwa lengo la
kujipatia chakula na baadhi yao walienda
maliwatoni akiwemo marehemu huyo .
Msaada: . ..Kijana huyo akitolewa kwenye
basi baada ya kujichinja kwa sime.
Walisema kwamba marehemu huyo ambaye
jina lake halikupatikana mara moja ,
wakati wa kushuka hakuonekana na kisu
aina ya sime lakini baadaye abiria
wachache waliotangulia kwenye gari ,
walimshuhudia akiwa ameshika sime hiyo
mkono pasipokujua aliipata wapi.
“Hata sisi tulishangaa kumuona akiwa
karibu na usukani wa dereva huku
akizamisha sime tumboni kisha kuichomoa
na kujichinja shingoni hadi pale alipokuwa
akivuta koromeo na kuning’ inia .
Damu kila mahali : . .. Akiingizwa katika gari
lingine huku damu zikiwa zimetapakaa.
“Tulichanaganyikiwa kwani ni kitu ambacho
hatukukitarajia na wala hatujawahi
kushuhudia tukio kama hilo la mtu
kujichinja hadharani , tulibakia kutokwa
machozi huku akina mama wakipiga yowe ,
hakuna mtu aliyethubutu kumsogelea
kumuokoa kwani kila mmoja alimuogopa.
“Tulishindwa kupanda basi hilo kwani ni
tukio la ajabu pia ndani kwa mbele
kulikuwa kumetapakaa damu , ghafla
alidondoka chini ndani ya gari , aliomba
kalamu na karatasi ili kuandika ujumbe.
Silaha: Polisi akiwa na sime aliyotumia
kujichinja kijana huyo .
“Dereva alichukua kalamu na kipande cha
karatasi na kumpa , alianza kuandika huku
damu ikimbubujika tumboni na shingoni,
hatukujua alichokiandika , aliishiwa nguvu
taratibu akadondoka .
“Abiria walimsogelea na kumuinua na
walimueleza kuwa atubu kwa Mungu kosa
alilolifanya kabla hajafa , alipiga magoti
na kuomba, ghafla alidondoka tena .
Imani: Kijana akisali kabla ya kukata roho.
“Kaka yake ambaye alikuwa akisafiri naye
kuelekea Dar es Salaam alichanganyikiwa
kwani hakutegemea kuwa mdogo wake
angejiua , kwani alisema hana historia ya
kuugua ugonjwa wa akili. Polisi walipigiwa
simu na walifika kumchukua lakini baada
ya muda mfupi akawa amefariki dunia .
“Sisi abiria wengine tuliendelea na safari
kuelekea Dar es Salaam ambapo marehemu
na kaka yake walibakia huko mkoani Lindi .
Kifo: .. .Kijana huyo baada ya kukata roho.
“Mara tulipofika Dar es Salaam dereva
alitusihi tukae kimya kwa dakika moja na
kuomba kutokana na tukio lililotupata,
tulifanya hivyo baadaye kila mmoja
alitawanyika na kuelekea kwake, ” kilisema
chanzo kwa sharti la kutoandikwa jina
gazetini .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi , ACP
Renatha Mzinga alipoulizwa mwishoni mwa
wiki iliyopita kuhusiana na tukio hilo alikiri
kutokea.
“Ni kweli tukio hilo lilitokea lakini kwa sasa
sina data kwani nipo njiani nikitokea
Nairobi, Kenya kikazi kuelekea Lindi , mara
nitakapofika huko ofisini ndipo nitapata
tukio zima lilivyokuwa, ” alisema Kamanda
Mzinga.

No comments:

Post a Comment

.