Tuesday, March 4, 2014

BILIONEA ANASWA KWA UNGA DAR


BILIONEA maarufu jijini Dar es Salaam , Ali
Khatibu Haji ‘Shkuba’( 44 ) ambaye alikuwa
akisakwa kwa muda mrefu na Kikosi
Maalum cha Polisi Tanzania kwa madai ya
kujihusisha na biashara haramu ya ‘unga ’,
amenaswa.
Bilionea Ali Khatibu Haji ‘Shkuba’( 44 )
aliyenaswa na polisi .
Vyanzo vililiambia gazeti hili kwamba ,
mtuhumiwa huyo alikamatwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA ) jijini Dar, Februari 23, mwaka huu ,
saa sita mchana akijianda kwenda nchini
Afrika Kusini .
Kwa mujibu wa chanzo hicho , mara baada
ya Shkuba kukamatwa alisafirishwa usiku
huohuo kwenda mkoani Lindi chini ya ulinzi
mkali wa polisi ambapo Februari 27 , mwaka
huu aliunganishwa na watuhumiwa wengine
na kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda
ya Kusini .
Madawa ya kulevya .
Shkuba ambaye ni mkazi wa Mikocheni , Dar
ni mfanyabiashara mwenye maduka ya
kubadili fedha (bureau de change) jijini,
ana makampuni ya ulinzi na nyumba
Mikocheni pia anamiliki magari ya kifahari
likiwemo aina ya Jeep lenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 150.
Vyanzo hivyo vilisema mtuhumiwa huyo
alikuwa akisakwa na kikosi kazi tangu
Januari 12 , 2012 na inadaiwa kwamba
alikimbilia nje ya nchi na kurudi kwa siri
na ndipo jeshi hilo liliamua kumuwekea
mtego.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa, tangu
vita ya kuididimiza biashara ya unga ianze
nchini, hakuna bilionea aliyewahi
kukamatwa zaidi ya mtuhumiwa huyo .
Gari aina ya Jeep lenye thamani ya zaidi
ya milioni 150 ambalo ni mojawapo ya
magari ya kifahari anayomiliki Shkuba.
Vyanzo vingine vya habari toka ndani ya
jeshi hilo vinadai kwamba, Shkuba aliwahi
kukamatwa mwaka 2006 kwa kuhusishwa na
biashara hiyo haramu na kuwekewa ulinzi
wa kifungo cha nje .
Habari zinadai kuwa, Januari 12 , 2012,
kikosi kazi cha kupambana na biashara hiyo
kilipata taarifa ya kuwepo kwa madawa
hayo aina ya heroin kiasi cha kilo 211 yenye
thamani ya shilingi bilioni 9 .4 mkoani Lindi
yakiwa tayari kusafirishwa nje ya nchi .
Kikosi hicho kiliweka mtego maeneo ya
Machinga Two mkoani humo na kufanikiwa
kukamata unga huo uliokuwa umefichwa
katika hoteli moja .
Binti wa Liyumba, Maureen Liyumba, siku
alipokamatwa pamoja na wenzake wakiwa
na madawa ya kulevya yenye thamani ya
shilingi bilioni 9 . 4 mkoani Lindi yakiwa
tayari kusafirishwa nje ya nchi.
Watu wanne walikamatwa sanjari nao ,
akiwemo binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa
Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ,
Amatus Liyumba, Maureen Liyumba ambaye
yuko mahabusu mpaka sasa na ameungana
na Shkuba.
Vyanzo hivyo vilidai kwamba watu hao
walikuwa wakiwasiliana na Shkuba ambaye
watuhumiwa walimtaja na ndipo polisi
walipoanza kumfuatilia .
Madawa ya kulevya aliyokamatwa nayo
binti wa Liyumba na wenzake .
Siku moja nusura polisi wamkamate ambapo
alikimbia na kulitelekeza gari lake aina ya
Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili
T 921 BPY ambalo bado linashikiliwa katika
Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Lindi .
Inadaiwa kwamba polisi walipokwenda
nyumbani kwake jijini Dar walimkosa na
kila walipopiga simu zake zilikuwa
hazipatikani hewani lakini baada ya
kumkamata walimpeleka Lindi kwa
helikopta .
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kudhibiti na
Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa
juzi na Uwazi kuhusu madai hayo
alithibitisha kukamatwa kwa Shkuba na
kwamba tayari ameunganishwa na wenzake
mkoani Lindi na wanaendelea kuwasaka
mabilionea wengine ndani na nje ya nje ya
nchi.
Maureen Liyumba pamoja na watuhumiwa
wenzake .
“Ni kweli tulikuwa tukimsaka kwa muda
mrefu Bwana Shkuba na tulijipanga vizuri
sisi kikosi kazi hali iliyotufanya tumnase .
“Hii vita ya biashara haramu kwa sasa si
kwa Tanzania tu bali ni vita ya dunia
nzima, nawaomba wananchi wazidi kutupa
ushirikiano na tutayafanyia kazi kwa siri
maelezo yao, ” alisema Kamanda Nzowa .

No comments:

Post a Comment

.