Saturday, March 1, 2014

OSTAZ JUMA"WASANII NA WATANGAZAJI WANA NJAA SANA..MTAKUFA NJAA"


Ostaz Juma ameendelea kuongezea petroli
kwenye moto aliouwasha jana. Na sasa
amewaamkia wasanii na watangazaji wote wa
redio nchini akisema njaa inawasumbua na
ndio maana wamekuwa wakimsujudia..
Hiki ndicho alichokiandika kwenye Facebook:
Naona watu mmeguswa sana mimi kuanika
Picha za PNC katika mitandao et, tatizo
wasanii wa tanzania mnanjaa sana kuanzia
watangazaji Radio na wasanii njaa ndio
zinazo wasumbua.
Hata mkisema napata pesa kwa utapeli
mitandaoni sawa ila ndio pesa zangu na ndio
zinawafanya mnitetemekee na kunitaja kwenye
vinyimbo vyenu visivyokua na ubora. Sawa mimi
tapeli naibia watu hilo sikatai nakubali mimi
tapeli ila imekuaje msanii wenu kaja kunipigia
magoti?
Wasanii wa bongo njaa sana na mtakufa na
njaa zenu. Acheni muendelee kunyonywa kwa
ujinga wenu shule mmezikimbia tatizo.
Mnaniona mimi mbaya kuweka picha Za PNC
zimewauma sana eeh. Hahahahahahahahahah
pesa inaongea hata mseme nini.
Naomba nyie mabloger na watangazaj msio kua
na taaluma wekeni na hii.

No comments:

Post a Comment

.