Saturday, March 1, 2014

MASKINI AFANDE SELE


SIKU chache baada ya kuzagaa kwa taarifa
za kuachana na mkewe mama Tunda ,
mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘ Afande
Sele’ ameibuka na kusimulia mambo ya
kusikitisha waliyopita katika safari ya
maisha yao.
Mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘ Afande
Sele’.
Akizungumza na wanahabari wetu ndani ya
Ukumbi wa Meeda, Sinza- Mori, Dar, juzi
Afande alisema hadi kufikia hatua ya yeye
kutangaza kuwa ameachana na mama
Tunda ambaye amedumu naye kama mume
na mke kwa zaidi ya miaka 10, alikuwa
akivumilia mambo mengi na mwisho kuamua
kuachia ngazi .
Afande Sele akiwa na familia yake .
“Nilikuwa nikielezwa mengi kuhusu mke
wangu, nilishapigiwa simu na kuambiwa mke
wangu anagombaniwa na wanaume usiku
klabu lakini huwa mimi siyo mtu wa kuishi
kwa hisia, nilivumilia nikiamini
atajirekebisha, haikuwa hivyo.
“Japo sikuwa na uthibitisho wa moja kwa
moja , lakini nyumbani alikuwa siyo mtu wa
kutulia, amekuwa akinizunguka hadi kwa
washkaji zangu wa karibu . Kuna jamaa
alichoshwa na habari hizo akanifuata na
kuniambia hata kama lakini uvumilivu
wangu ulizidi , ” alisema Afande kwa hisia.
Akiendelea kushusha masikitiko yake mbele
ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi,
Afande alienda mbele zaidi kwa kusema
mbali na mkewe huyo kumsaliti kwa
wanaume tofauti wakiwema marafiki zake,
ilifika wakati mama Tunda akawa
anachukua fedha ndani na kwenda kutumia
na wanaume .
Alisema alitumia mwanya wa mkali huyo wa
mashairi anapokuwa amesafiri katika shoo
mbalimbali na kuachiwa fedha za matumizi
pamoja na ujenzi wa nyumba yao mpya,
kutanulia.
“We acha tu , yaani fedha za matumizi ,
ujenzi nilikuwa namuachia lakini cha
kusikitisha ni kwamba alizitumia kutanulia,
jambo ambalo nililizidi kunitia umaskini na
machungu ukizingatia jamii inaniheshimu
kama msanii , mbaya zaidi wananchi
wamenitaka nigombee ubunge Morogoro
Mjini, ” alisema Afande .
Akizidi kushusha ‘ vesi’ , Afande alitiririka
kuwa kuna wakati aliwahi kupewa taarifa
na rafiki yake mwingine aishie Kurasini
jijini Dar ambaye alilamika juu ya mkewe
kufika kwa jamaa huyo na kuazima fedha
bila kuzilipa .
Kwenye aya nyingine, mkali huyo alisema
anakumbuka jinsi alivyoishi na familia
yake, mkewe, wanaye Tunda na Ahsante
Sanaa lakini hana jinsi kwani ameona bora
kuachana kwani umri wake una mruhusu
kuoa mke mwingine siku ikitokea .
“Nakumbuka maisha kidogo ya furaha na
familia, mama Tunda atabaki kuwa mama
wa watoto wangu lakini kamwe hawezi
kurudi kwangu kwani itakuwa ni aibu juu ya
aibu , ” alisema.
Afande aliachana na mama Tunda mwishoni
mwa mwaka jana alipotimba jijini Dar
katika shughuli zake za kikazi na
kumuachia mkewe fedha za ujenzi lakini
aliporejea nyumbani Morogoro, alikuta
mzazi mwenzake huyo ameondoka nyumbani
na kuacha funguo, kila alipompigia simu
hakupokea.
Alipoulizwa kuhusiana na shutuma
zilizoporomoshwa na Afande, mama Tunda
alitiririka:
“Alinipa Sh . milioni 3 za shoo tu, tukanunua
vifaa vya ujenzi lakini siyo kwamba
nilitanua na wanaume , tena kama ni
kumfumania , mimi ndiye nilimkuta na
mwanamke alitoka naye Fiesta Dodoma,
sikutaka tu kumsema, hizo taarifa
anazusha tu.
“Kwanza kuna mambo mengi tu
amenifanyia, alikuwa mlevi kwani hadi
wazazi wangu walikuwa wakinishangaa
sana, sasa na mimi nikaona bora niachane
naye, ” alisema mama Tunda .

No comments:

Post a Comment

.