Monday, March 3, 2014

RIPOTI KAMILI


MASKINI! Stori zilizozagaa mitaani kuhusu
mali za aliyekuwa mkali wa sinema za
Kibongo, marehemu Steven Kanumba
zinasema kuwa , zimeuzwa na kampuni
aliyoiacha, Kanumba The Great Film
imefilisika, Ijumaa Wikienda linakupa
ripoti iliyoshiba .
Marehemu Steven Kanumba .
Habari zinadai kuwa baada ya kifo cha
Kanumba Aprili 7 , 2012, mali alizoziacha
zinafujwa, hakuna utaratibu mzuri wa
kusimamia mamb
na kwamba , uzalishaji wa sinema katika
kampuni yake ni mdogo tofauti na enzi za
uhai wake .
Chanzo chetu cha habari ambacho ni mmoja
wa wasanii wa filamu Bongo aliye na
ukaribu na familia hiyo , alisema ni kweli
kuna tatizo la usimamizi na uendelezaji wa
mali za marehemu lakini akasema ni jambo
la kawaida kwa sababu marehemu
ameondoka na mbinu zake.
Ofisi ya Kanumba ya Sinza Mori, Dar.
“Kila mtu ana nyota yake kaka,
asikudanganye mtu, lakini pia kila mmoja
ana namna anavyojua kuendesha biashara
zake, sasa Kanumba alikuwa na mikakati
yake, hawa walioachiwa nao wana mikakati
yao. Mfano , hawataweza kutoa sinema
nyingi kwa sababu soko la waliobaki si kubwa
kama ilivyokuwa kwa Kanumba .
“Angalia hata ushindani. .. hivi kweli Seth
(Bosco , ‘ mdogo wa Kanumba ’) anaweza
kupambana na magwiji kama JB ( Jacob
Steven ) au Ray (Vincent Kigosi) sokoni ?
Watu waache lawama, ” alisema msanii huyo
ambaye aliomba hifadhi ya jina .
Marehemu Kanumba enzi za uhai wake
akiwa pembeni ya gari lake .
MDOGO WAKE ABANWA
Waandishi wa habari hizi walifunga safari
hadi Sinza –Mori, Dar zilipo Ofisi za
Kanumba The Great Film na kuzungumza na
mdogo wa marehemu Kanumba , Seth Bosco
ambaye alisisitiza kampuni ya marehemu
kaka yake haijafilisika kama maneno
yalivyozagaa mitaani.
“Hao wanaosema eti kampuni ya Kanumba
imefilisika wanakurupuka tu, hawana cha
kufanya lakini nataka kuwahakikishia
kuwa, hatujayumba ila tunakabiliwa na
changamoto za kawaida tu kama
inavyokuwa kwa kampuni nyingine, ” alisema
Seth.
Toyota Hiace aliyokuwa anamiliki Kanumba .
HIACE, TOYOTA GX 110
WIKIENDA : Lakini Seth kuna maneno kuwa
lile gari aina ya Toyota GX 110 na Toyota
Hiace lilikokuwa likitumika kwenye kurekodi
sinema yameuzwa , ni kweli ?
SETH: Ni kweli Hiace tumeiuza lakini
tumenunua Noah kwa kazi hiyohiyo ya
‘location ’, kuhusu GX 110 halijauzwa , lipo
nyumbani hata sasa hivi ukienda utalikuta .
KUHUSU LEXUS
WIKIENDA : Tulisikia gari alilokuwa
akitembelea marehemu Kanumba , Toyota
Lexus limeuzwa. Ni kwa nini na liliuzwa kwa
bei gani?
SETH: Kama familia tuliamua kuliuza kwa
sababu ya gharama za uendeshaji . Lile gari
linatumia mafuta mengi sana na
matengenezo yake ni makubwa na
hatukuona sababu za kuingia kwenye
gharama kubwa za namna hiyo .
Kuhusu bei lililouziwa, kwa kweli sifahamu.
Kama unavyojua baada ya mtu kufariki
dunia, huwa kuna msimamizi wa mirathi ,
yeye ndiye anayejua kuhusu hilo .
Mama mzazi wa Kanumba , Flora Mtegoa .
UZALISHAJI
WIKIENDA : Kipindi cha Kanumba , alikuwa
akitoa sinema nyingi sana , nadhani kama
sikosei ilikuwa moja kila baada ya miezi
miwili wakati mwingine kila mwezi sinema
moja lakini baada ya yeye kuondoka ,
uzalishaji hakuna tena .
Mfano mpaka sasa kuna sinema mbili tu
sokoni tangu alipokufa ambapo inakaribia
miaka miwili sasa. Tatizo ni nini?
SETH: Ni kweli , lakini si kwa sababu ya
tatizo la fedha – ni uhitaji . Unajua kuna
changamoto nyingi sana kwenye tasnia yetu .
Ni kweli mpaka sasa tumetoa sinema mbili;
Malaika na Wonderful Girl ambayo tayari
iko kwa msambazaji lakini bado haijaingia
mitaani.
Mwaka huu ndiyo tumeanza, kuna kazi
moja tunaifanya sasa hivi, ingawa si ya
kwetu, sisi tunasimamia kwenye production
(kuizalisha ) lakini mipango ya mwaka huu
ni mikubwa , mapema sana , tutaanza
kurekodi kazi yetu nyingine , kwa sasa siwezi
kusema jina lake ila inakuja .
Mdogo wa marehemu Kanumba , Seth Bosco.
OFISI VIPI ?
WIKIENDA : Kwa nini muda mwingi ofisi
inakuwa imefungwa tofauti na ilivyokuwa
kwa marehemu Kanumba ?
SETH: Kaka hii ni kampuni , sisi tunafanya
biashara na mteja wangu hahitaji
kunifuata . Mimi mteja wangu ni Steps ,
ambaye namtayarishia kazi kisha
nampelekea.
Milango inaweza kuwa imefungwa lakini
kazi za ‘editing ’ zikawa zinaendelea ndani
au tukafunga ofisi lakini tukawa location
tunarekodi, kuna tatizo gani hapo ?
WIKIENDA : Lakini marehemu alikuwa
anauza hadi filamu hapa ofisini ?
Imekuwaje siku hizi?
SETH: Hatujawahi kuuza sinema hapa ofisini
ila tulikuwa tunaweka kama mfano wa kazi
zilizowahi kufanywa na marehemu – si za
watu wala kampuni nyingine . Lengo lilikuwa
kuwapa watu wanaotutembelea ( bure) , si
kwa kuwauzia .
Bila shaka maelezo hayo ya Seth yatakuwa
yamejibu maneno yote yanayosemwa
mitaani.

No comments:

Post a Comment

.