Monday, March 3, 2014

MWEE! ETI KISA CHA KAJALA KULISHWA SUMU NI MUME WA MTU


Wiki iliyopita muigizaji wa filamu nchini Kajala
Masanja alikiri kuwekewa sumu wakati
alipokuwa kwenye show ya mwanamuziki Izzo
Buzness. Star huyo aliwahi hospitalini na hali
yake kuwa nzuri. Hata hivyo star mmoja wa
filamu akizungumza na Swahiliworldplanet kwa
sharti la kutoandikwa jina lake alisema kuwa
Kajala alifanyiwa kitendo hicho cha kifedhuli
kutokana na madai ya kutembea na mume wa
mtu ambaye anadaiwa kumpangishia nyumba
ya kifahari "kachukua mume wa mtu huyo
Kajala, yes kuna libaba limempangia nyumba
nzima so nahisi ndiyo sababu ya kuwekewa
sumu" kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo Kajala alijaribu kutafutwa ili
kutolea ufafanuzi madai hayo lakini kwa siku
mbili hakuweza kupatikana.

No comments:

Post a Comment

.