Thursday, December 5, 2013

AJIUA BAADA YA KUMTUMIA MUMEWE MESEJI YA MPENZI WAKE


Marehemu Gail Crocker wakati wa uhai wake.
POLISI mwanamke nchini Uingereza, PC Gail
Crocker (46), alijiua siku za karibuni baada ya
kuandika ujumbe mfupi wa simu (meseji) kwa
mpenzi wake akimshukuru kwa “burudani”
waliyofaidi walipokutana kwa siri – lakini, kwa
bahati mbaya, aliituma meseji hiyo kwa
mumewe.
Katika meseji hiyo, Crocker aliandika kwamba:
“Ningependa tuwe tunafanya hivi kila mara.”
Tukio la wawili hao lilitokea wakati mumewe
Crocker akiwa safarini kibiashara.
Uchunguzi uliofuatia tukio hilo la kujiua kwa
Crocker ulibaini kwamba baada ya mumewe
kurejea nyumbani huko St Stephen, Cornwall,
ulizuka ugomvi na mwanamke huyo mwenye
watoto wawili alikunywa vidonge vingi na
kufariki.
Na mumewe, Peter Crocker (49) alisema: “Gail
alikuwa ndiyo maisha yangu.”

No comments:

Post a Comment

.