DAKIKA za mwisho za maisha yake, Rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,
hakuwa akitumia mashine ya kumsaidia
kupumua.
Mmoja wa wanafamilia wa Mandela, Bantu
Holomisa, aliyemuona kiongozi huyo dakika
90 kabla ya kifo chake, ameripotiwa akisema
alikuwa akipumua bila msaada wa mashine
hiyo na alikuwa amezungukwa na
wanafamilia wa karibu.
“Wakati anafariki Alhamisi iliyopita usiku,
hakuwa akitumia msaada wa mashine
kupumua, alikuwa akipumua bila mashine
hiyo,” alisisitiza mtoa taarifa aliyenukuliwa
na gazeti la kila wiki la Sunday Times.
Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na mapafu,
amekuwa akilazwa mara kwa mara kutokana
na matatizo hayo na ni mara chache alikuwa
akilazimika kutumia mashine ya kumsaidia
kupumua.
Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times,
Mjukuu wa Mandela, Mandla aliitwa kwa
dharura kutoka katika kijiji alikozaliwa
Mandela, Mvezo ili awe karibu na babu yake
na alibaki hapo mpaka alipovuta pumzi ya
mwisho.
Mbali na Mandla, wengine waliokuwepo
wakati akikata roho ni viongozi waandamizi
wa chama cha ANC na viongozi wa dini
waliokuwa wakijitahidi kufariji familia na
marafiki wa karibu.
Kwa mujibu wa jarida la kila wiki la City
Press, wanafamilia wa karibu waliruhusiwa
kuingia katika chumba cha Mandela wawili
au watatu kwa ajili ya kuonana naye kwa
mara ya mwisho.
“Waliokuwa nyumbani wamezungumzia
huzuni kubwa iliyokuwa katika nyumba hiyo,”
City Press liliandika.
Ilielezwa pia kwamba Mandela alikuwa
hajaweza kuzungumza neno kwa miezi
kadhaa. Gazeti la Sunday lilimnukuu Bantu
Holomisa, ambaye ni mmoja wa watu
waliomuona Mandela katika dakika za
mwisho, akisema alipokea simu akielezwa
kuwa hali ya kiongozi huyo ilikuwa mbaya.
“Nilikwenda moja kwa moja kumuona katika
chumba chake, Nilihuzunika kumuona katika
hali ile kwa kuwa alikuwa amebadilika tangu
nilipomuona mara ya mwisho,“ alisema.
Holomisa alisema alikaa kwa zaidi ya saa
moja na Mandela na kuondoka nyumbani
hapo dakika 90 kabla ya kifo chake kutokea.
“Familia ilikuwa inajitahidi kuvumilia na
kulikuwa na utulivu.
Hali ilikuwa ngumu pale wanajeshi
walipowasili kuchukua mwili wa Madiba
karibu saa sita za usiku,” gazeti hilo
lilimnukuu mmoja wa wanafamilia
aliyekuwepo.
Sunday, December 8, 2013
Aliyemuona Mandela dakika 90 kabla ya kifo asimulia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment