PICHA ya mwisho ya Kiongozi wa zamani
wa Afrika Kusini, Nelson Mandela akiwa hai
imetolewa akionekana mwenye tabasamu
huku ameshika mkono wa kitukuu chake.
Picha hiyo ilipigwa Mei nyumbani kwake
Houghton jijini Johannesburg akiwa amekaa
kwenye kiti alichokipenda sana –mwezi
mmoja kabla hajalazwa hospitalini jijini
humo. Kwa familia ya Mandela picha hiyo
inabaki kuwa kumbukumbu nzuri za nyakati
za furaha.
Na kwa mtoto wa miaka mitatu, Lewanika,
ambaye anaonekana kwenye picha hiyo,
itakuwa ni kumbukumbu ya aina yake,
anasema baba yake, aliyeipiga, akiongeza
kuwa kitakuwa ni kitu ambacho ni hazina
kwake atakapokuwa amekua kiasi cha
kuweza kuelewa mambo.
Ni taswira ya mwisho ya mtu wa kihistoria
ambaye Waafrika Kusini na walimwengu
duniani wanamwomboleza- huku pia
wakisherehekea urithi aliowaachia wa amani,
mtu mashuhuri ambaye karama zake
zitahisiwa na kila mtu duniani hata katika
miaka ijayo.
Picha hiyo inamwonesha Lewanika akiwa
amekaa kwenye mkono wa kiti, huku
akimwangalia kwa udadisi mkubwa babu
yake, mtu ambaye amekuja kuwa alama ya
nchi yake, katika mapambano dhidi ya
maovu, lakini ambaye pia mtoto huyo alizoea
kumwita ‘baba’.
Akihojiwa jana na The Mail on Sunday la
Uingereza, baba yake Lewanika, Ndaba
Mandela-ambaye ni mjukuu wa Mandela-
alisema alipiga picha hiyo akiamini kuwa
huenda ikawa ni fursa yake ya mwisho
kuwapiga picha wawili hao wakiwa pamoja.
“Ilikuwa Mei, Jumamosi moja mchana.
Tulikuwa tumekuja kumjulia hali mzee huyo
na tukamkuta akiangalia kipindi cha National
Geographic kwenye televisheni, “Ndaba (30)
alisema. “Alimwangalia Lewanika na
kumwita, “njoo, njoo.” Uso wa mzee ulijawa
nuru alipomwona-kama ujuavyo alipenda
sana watoto. Walikumbatiana na mwanangu
akamwita “baba”.
Ilinigusa sana kuwaona wawili hao wakiwa
pamoja.” Ndaba ambaye ni Mwenyekiti wa
Wakfu wa Africa Rising ambayo
inashughulikia maendeleo ya uchumi wa
vijana wa Afrika Kusini, anaishi katika
nyumba ya Mandela ya Houghton, ambako
ndiko mzee huyo alifia Alhamisi. Ndaba
alisema: “Tunajivuna kwamba tumeweza
kutunza kumbukumbu hii maalumu na
kupata heshima ya kuionesha dunia.”
Alipenda watoto Binti wa Mandela, Zindzi
(53) naye aliiambia The Mail on Sunday
mapema mwaka huu jinsi baba yake
alivyopenda kuwa na watoto na vijana karibu
naye.
Anakumbuka simulizi ya jinsi alivyotoka
gerezani, alipomwomba aache
kumnyonyesha mwanawe wa kiume ili akae
na mtoto huyo chumbani kwake, amlishe na
kumlea kila usiku. Zindzi alisema wakati
fulani:”Baba hufurahi sana anapoona watoto
wamemzunguka. Anawapenda na hufurahi
wakimpandapanda.”
Picha hii ilitoka wakati Mandela
akisumbuliwa na maambukizi sugu ya
mapafu yaliyogundulika akiwa gerezani
alipotengwa na kuwekwa kwa miezi kadhaa
akiwa ndani ya rumande yenye giza.
Sunday, December 8, 2013
Picha ya mwisho ya Mandela yaoneshwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment