Sunday, December 8, 2013

ARSENAL YASHIKWA EPL, YALAZIMISHWA SARE YA 1- 1 NA EVERTON


Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la
kuongoza katika dakika ya 80 ya mchezo .
Ozil akishangilia na wachezaji wenzake
baada ya kufunga bao .
Gerard Deulofeu wa Everton ( kushoto)
akishangilia bao la kusawazisha dakika ya
81 ya mchezo .
Beki wa Arsenal Laurent Koscielny ( kushoto)
akijaribu kumzuia Steven Pienaar wa Everton
wakati wa mchezo huo.
Timu ya Arsenal imeshikwa baada ya kutoka
sare ya 1- 1 na Everton katika mechi ya Ligi
Kuu England iliyopigwa Uwanja wa Emirates
jijini London , Uingereza hivi punde.
Bao la kuongoza la Arsenal limewekwa
kimiani na Mesut Ozil dakika ya 80 kabla ya
Gerard Deulofeu kusawazisha bao hilo dakika
ya 84 na kufanya matokeo kuwa 1- 1.
Mpaka mwisho wa mchezo Arsenal 1 na
Everton 1. Kwa matokeo hayo bado Arsenal
wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 35
wakati Everton wapo nafasi ya tano wakiwa
na pointi 28.

No comments:

Post a Comment

.