Sunday, December 8, 2013

BAADA YA KIPIGO CHA NEWCASTLE: SHABIKI WA MAN UNITED AJIUA KWA KUJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA SABA


Kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa
Manchester United Football Club amejiua jana
usiku jijini Nairobi baada ya timu yake
kufungwa 1-0 to Newcastle.
Polisi imesema kwamba John Jimmy Macharia,
23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya
kujua timu yake imepoteza mchezo wa jana
jioni. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jiji la
Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia
rafiki zake hawezi kuendelea kuangalia timu
yake ikifungwa kila siku kabla ya kuruka
ghorofani. “Mashahidi wote waliokuwepo wakati
wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi
wanahojiwa,” alisema. Kibue aliwashauri vijana
wa jiji la Nairobi kufahamu English Premier
League ni mchezo tu kama ilivyo michezo
mingine na hivyo waache kuchukua hatua za
namna hii kisa michezo. Hii si mara ya kwanza
kwa kwa kijana kupoteza maisha kwa ajili ya
michezo inayochezwa England,” alisema Kibue
-Shaffidauda

No comments:

Post a Comment

.