Ni mashabiki wachache wa Manchester United
wanaikumbuka siku ile ambayo timu yao
ilishushwa daraja. Ilikuwa msimu wa 1973/74 na
mechi ya mwisho ya ligi ilikuwa tarehe 27 Aprili
1974. Kwa mashabiki wa Manchester United
wataikumbuka tarehe 27 April 1974 kama "the
worst day in the history of football". Kwa
wasioipenda Manchester United, wanaikumbuka
hiyo tarehe kama "the best day in the history of
football." Kwa mara ya kwanza Manchester
United ilishushwa daraja baada ya kucheza
kwenye ligi daraja la kwanza kwa miaka 36.
Lakini huwezi kuongelea tarehe 27 April 1974,
siku ambayo Manchester United ilishishuka
daraja, bila kumwongelea Denis Law. Denis Law
ni legend Old Trafford. Alijiunga na Manchester
United mwaka 1962 akitokea Manchester City.
Aliichezea Manchester United kwa muda wa
miaka 11, ambapo alifunga magoli 237 kwenye
mechi 404 alizocheza. Mashabiki wa Manchester
United walimwita “The King” na “The Lawman”.
Itakumbukwa pia kuwa Manchester United
ilikuwa ikisuasua kwenye ligi baada ya timu
kupata ajali ya ndege Munich Ujerumani mwaka
1958 ambapo abiria 20 kati ya 44 walipoteza
maisha. Kati ya abiria 20 waliofariki, saba
walikuwa wachezaji wa Manchester United. Kwa
hiyo, baada ya ajali hiyo, Manchester United
ilikuwa wanapambana mara nyingi kuepuka
kushuka daraja.
Baada ya kuichezea Manchester United kwa
miaka 12, Denis Law alihamia Manchester City
msimu wa 1973/74 bila ada (free transfer).
Manchester United walikuwa hawamhitaji tena
maana kiwango chake cha mpira kilikuwa
kimeshashuka na umri pia ulikuwa umesogea.
Pia George Best na Bob Chalton walikuwa
wameshaondoka.
Katika mechi ya mwisho ya ligi msimu wa
1973/74, Manchester United ilicheza na
Manchester City Old Trafford. Manchester United
ilitakiwa kushinda ile mechi ili isishuke daraja.
David Law alicheza lakini tokea mwanzo
alionekana kutokuwa na raha maana kama timu
yake kipenzi (Manchester United) ingefungwa
basi ingeshushwa daraja.
Mpaka dakika ya 80 mechi ilikuwa bila bila.
Mnamo dakika ya 81, Denis Law aliifungia
Machester City goli kwa kisigino. Lilikuwa goli
zuri na tamu lakini siyo kwa mshabiki yoyote wa
Manchester United. Denis Law mwenyewe
hakushangilia kwa kufikiri kuwa goli lake la
kisigino lingeishusha daraja Manchester United.
Mara tuu baada ya kufunga like goli, alibadiliswa
huku akitoka uwanjani akiwa ameinamisha
kichwa chini kwa masikitiko makubwa ya
kuishusha daraja Manchester United.
Baada ya Denis Law kutoka uwanjani, mashabiki
wa Manchester United walivamia uwanja na
kumlazimisha refa kumaliza mechi katika dakika
ya 85. Siku chache baadae, chama cha mpira
kilifanya mapitio ya mechi ile na kusimama na
matokeo ya mechi. Kwa hiyo, Manchester City
ikawa imeshinda bao moja lililofungwa na Denis
Law kwa kisigino na Manchester United
kushushwa daraja.
Hata hivyo, ilikuja kugundulika baada ya mechi
kuwa bado Manchester United ingeshuka daraja
bila kutokana na matokeo ya ile mechi. Hii
ilitokana na matokeo ya kwenye mechi nyingine
za mwisho zilizochezwa siku ile. Lakini Denis
Law aliamini kabisa kuwa goli lake la kisigino
limeishusha daraja Manchester United.
Msimu uliofuata (1974/75) Manchster United
ilicheza kwenye ligi ya daraja la pili na
kufanikiwa kurudi tena ligi ya daraja la kwanza
katika msimu wa 1975/76.
Sunday, December 8, 2013
Je! WAJUA SIKU MANCHESTER UNITED ILIPOSHUSHWA DARAJA..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment