Erick Evarist na Sifael Paul
ACHANA na mabifu yaliyotangulia , hili ni
jipya kabisaa ! Msanii wa sinema na Bongo
Fleva , Baby Joseph Madaha ameingia kwenye
bifu zito na Nasibu Abdul Jumaa ‘ Diamond
Platnumz’ na kudai staa huyo wa Wimbo wa
Number One ni mzinzi ‘ fuska’ , Amani lina
mkanda mzima .
Baby Madaha akiwa na Diamond.
Bila kumung ’ unya maneno , mapema wiki hii ,
Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni
Rais wa Wasafi Classic Baby ( WCB )
akimtuhumu kuwa na tabia za kifuska .
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya
Diamond kamwe hauwezi kulingana na
mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya
kubebwa na skendo tu .
Diamond na Wema .
CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii , ilivuja posti
ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha
ikimpaka Diamond kuwa siyo mwanamuziki
kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye
uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba
wa THT .
Sehemu ya posti hiyo ilionesha kuwa ,
Diamond si msanii wa muziki bali ni mzinzi
f’ lani hivi anayefanya biashara ya muziki
kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania
watakapojitambua na kuacha kulewa penzi la
Diamond , huo ndiyo utakuwa mwisho wa
maisha yake kimuziki kwa sababu hatakuwa
na jipya na hivyo soko lake litaporomoka , ”
ilisomeka posti hiyo .
Diamond na Penny .
UKWELI NI UPI ?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini
na kuibuka kwa makundi mawili
yanayokinzana , Amani lilimtafuta Baby
Madaha ili kujua ukweli wa posti hiyo ndipo
akatiririka aya za kuthibitisha kuwa picha
haziivi, hamkubali Diamond na kudai hata
kimuziki hamkubali kwani anaamini wapo
wanamuziki wanaofanya vema katika gemu
kuliko yeye.
“… tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara
siyo mwanamuziki. Kuhusu hiyo posti iwe ni
mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi
hayo maneno yanamstahili kabisa . Mzinzi tu .
“Diamond anabebwa na media ( vyombo vya
habari) . Kuna wanamuziki wengi wazuri
sembuse yeye? Ana nini haswa ?” alihoji
Baby.
Diamond na Jokate .
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo ya Baby kwa
kifupi, Amani lilimuweka ‘ pending ’ kwa muda
na kumwendea hewani Diamond ili liweze
kujua upande wake analizungumziaje bifu hilo
ambalo lilikuwa likienea mitandaoni kama
moto wa kifuu.
Tofauti na matarajio ya mapaparazi wetu
kwamba huenda angejibu mashambulizi
makali kwa Madaha, Diamond au ‘ Sukari ya
Warembo’ aling’ aka huku akimponda
mwanadada huyo na kumshangaa :
BOFYA HAPA KUMSIKIA
“Daaah! Huko ni kunishusha … mimi na huyo
( Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi
kunilinganisha na mtu ambaye yupo chini
yangu sana , nikijibizana naye nitajishusha tu .
Ingekuwa ni mtu mkubwa mwenye levo yangu
hapo ningesema natakiwa kusema neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘ kiki’ tu kupitia
mimi, nipo na dili zangu za maana nipoteze
muda kwake? Atafute wa levo yake na wala
si mimi .”
UZINZI VIPI ?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi ambalo
Baby Madaha aliumaanisha katika posti yake,
Diamond aliendelea kukazia kuwa hana muda
wa kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha
ambaye kimsingi ni kama ardhi na mbingu .
“Huyo anatafuta kiki tu , aachane na mimi …
mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi
kwa wapi ?” alikazia Diamond a. k .a Weka
Mbali na Watoto Wazuri wa Kike .
BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu wakimalizana na
Diamond , kilongalonga kimoja cha paparazi
wetu kilikuwa kikionesha kinaita , ilivyokatika
ya Diamond , Baby akapanda hewani kwa
mara nyingine .
Safari hii alimchana laivu : “Nimeisoma upya
posti yenyewe , kilichopo humu ni ukweli
mtupu. Hakuna hata tone la uongo , wewe
utamlinganisha Diamond na mtu kama
Barnaba ? Huyu ni mfanyabiashara tu , hajui
kuimba kwa kutumia vyombo kama mimi .
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja
cha muziki atajiitaje mwanamuziki ?
Anastahili kabisa ujumbe huu. ”
UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga
swali Baby Madaha kuhusiana na ufuska
ambao ulikuwa umetajwa katika maelezo ya
awali , kama endapo Diamond ni mzinzi au
yeye ndiyo mzinzi .
Katika maelezo yake, Baby Madaha
aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja
namna gani anaweza kumuita Diamond
mzinzi . Sikia:
Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki,
je , suala la uzinzi ni nani analo kati yako na
yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi . Diamond ndiyo mzinzi
tena sana tu .”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi ?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake,
kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na
Jokate Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo. ”
Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na
wanaume tofauti ? Hujawahi kufumaniwa ?”
Baby: “Mimi sijawahi , yeye amewahi na
hakuwahi kukanusha hivyo inadhihirisha
kuwa ni kweli . Kwangu mimi kila aliyetajwa
kutoka na mimi kama haikuwa kweli ,
nilikanusha mara moja yeye mbona
hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na
nani?”
Baby: “Acha hizo , kwani hukumbuki kipindi
cha Wema ? Mara alinaswa na Aunt mara
na… yule ndiyo mzinzi sasa . ”
KWANI WALITONGOZANA ?
Kuhusu suala la kutongozwa , Baby alisema
Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi ,
alisema hata kama ikitokea siku staa huyo
akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia
kwani hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo
na si vitoto kama Diamond .
“Hana hela , kamwe siwezi kumkubalia . Ni
mtu ambaye ana vihela mbuzi sasa mtu
kama yeye mimi wa nini? Ndiyo maana
aliwahi kukimbiwa na mwanamke kwa kuwa
hana hela .
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo
mwenye hela , mimi na yeye ni mbalimbali
kabisa . Hata muziki ninaofanya hauwezi ,
mimi ninaimba RnB yeye anafanya Pop , tuko
tofauti kabisa , ” alisema Baby pasipo kumtaja
mwanamke aliyemkimbia Diamond .
TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi
na ‘ totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo
aliyemzingua aitwaye Sarah , Rehema Fabian,
Jacqueline Wolper , Upendo Mushi ‘ Pendo wa
Maisha Plus’ , Wema Sepetu , Natasha ( Video
Queen wa Wimbo wa Moyo Wangu ) , Najma
( aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue ) , Jokate
Mwegelo , yule demu wa Kenya na aliyekuwa
mwigizaji aliyefulia ambaye ni mke wa mtu.
Kwa upande wake Baby Madaha
anayekimbiza na ngoma yake ya Summer
Holiday naye si haba kwani aliwahi
kuripotiwa kuminya kimapenzi na yule mtoto
wa mwanasiasa maarufu Bongo ( jina lipo) ,
Mwisho Mwampamba , Dokta Pakir , Juma
Nature na Joe Kairuki aliye naye sasa
ambaye ni mume wa mtu.
Thursday, December 5, 2013
BABY MADAHA APASUA JIPU : DIAMOND FUSKA !
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mmmh yangu macho ctii neno hapooooooo
ReplyDelete