Thursday, December 5, 2013

WAFANYABIASHARA WAPIGWA RISASI, ARUSHA


Na Joseph Ngilisho, Arusha
MASKINI ! Wafanyabiashara wawili, wakazi
wa Tengeru, wilayani Arumeru mkoani hapa ,
Joel Zephania Mzava ( 35) na Gidiona Kija
Mfuru ( 43) , wamenusurika kuuawa baada ya
kupigwa risasi na watu wanaodaiwa ni askari
wa usalama barabarani.
Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu
katika Hospitali ya Wilaya ya Arumeru .
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo la
kusikitisha lilijiri hivi karibuni kati ya eneo la
Msitu wa Mbogo na Karangai wilayani
Arumeru, majira ya saa 4: 10 asubuhi ambapo
wafanyabiashara hao wa kiume walijeruhiwa
sehemu mbalimbali .
Gazeti hili liliwakuta watu hao wakiwa
wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Arumeru wakitibiwa majeraha makubwa
waliyoyapata.
Mashuhuda hao walisema kuwa ,
wafanyabiashara hao walikuwa kwenye gari
la mizigo aina Nissan Mitsubishi lenye namba
T 481 BGF wakitokea wilayani Simanjiro.
Kushoto ni mmoja wa majeruhi baada ya
kupatiwa matibabu .
Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo ,
mmoja wa majeruhi hao ambaye amepoteza
kipande kwenye sehemu nyeti baada ya
kupigwa risasi katikati ya miguu , alisema
waliomba lifti katika gari hilo wakitokea
Landabani , Simanjiro walikokuwa
wamepeleka biashara zao.
Alisema gari hilo lilikuwa na magunia 45 ya
mkaa, mali ya dereva wa gari hilo aliyetajwa
kwa jina moja la Dismack , mkazi wa Tengeru.
Mzava alisema walipopewa lifti walikaa
mbele na dereva hivyo wakawa watatu .
Alisema walipofika eneo la tukio waliwaona
askari wawili wamesimama pembeni ya
barabara kwenye kichaka wakiwa na pikipiki
aina ya Toyo .
Alisimulia kuwa askari hao waliwasimamisha .
Majeruhi akipatiwa huduma katika Hospitali
ya Wilaya ya Arumeru .
Baada ya kusisimama waliwatambua askari
hao wanaodaiwa ni wa Kituo cha Mbuguni
ambao walimtaka dereva kuwapatia kibali
cha kusafirisha mkaa .
Dereva alitoa kibali na risiti za malipo lakini
askari hao hawakuridhika na kutaka
wapatiwe fedha ndiyo waweze kumwachia
vinginevyo wangelipeleke gari kituoni .
Baada ya kuona usumbufu, dereva aliondoa
gari ndipo askari mmoja aliwamiminia risasi
zaidi ya 20 na kusababisha gari hilo
kuserereka na kupinduka huku damu zikiwa
chapachapa.
Katika tukio hilo wasamaria wema walifika na
kutoa msaada kwa majeruhi kwa kutafuta
gari na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi
Usa -River ambako walipatiwa hati ya
matibabu ( PF -3 ) kisha wakakimbizwa
hospitali hiyo ya Wilaya ya Arumeru.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru, OCD
Benedict Mapujila alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa tayari
ameshapeleke taarifa kwa mkuu wa polisi
mkoani hapa, RPC Liberatus Sabas .

2 comments:

.