Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ( kushoto) ,
Afisa Habari - Baraka Kizuguto na Beno
Njovu Katibu Mkuu mpya( kulia )
Mwenyekiti wa Young Africans Yusuf Manji
leo amemtambulisha rasmi Bw . Beno Njovu
kuwa katibu mkuu mpya wa klabu akichukua
nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua
kaimu katibu mkuu kwa kipindi cha mwaka
mmoja .
Akiongea na waandishi wa habari makao
makuu ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa
Yanga Bw. Yusuf Manji amesema Beno Njovu
anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia
leo na Mwalusako atakua nae pamoja kwa
kipindi cha mwezi mmoja mpaka
atakapokabidhi kazi rasmi .
Aidha Manji ametangaza mkutano mkuu wa
wanachama Januari 19 , 2013 ambapo
wanachama watapata fursa ya kupitia
mapato na matumizi, na ajenda zingine
mbalimbali ambazo zitajadiliwa katika
mkutano huo .
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi
mwishoni mwa wiki kimemteua Bw. Seif
Ahmed " Magari " kuwa Mwenyekiti wa Kamati
ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na
nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa
Kamati Kuu ya Utendaji wa klabu ya Yanga.
Katika mkutano na wandishi wa habari
makao makuu ya klabu Manji ametangaza
rasmi kutogombea tena uenyekiti katika
uchanguzi mkuu ujao , hili nimeliamua
mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa
nimefuata demokrasia .
Nina miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu
mwakani hivyo sasa ninajitahid kukamlisha
shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya
ndani ya Yanga nikiwa kama mwenyekiti ili
uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza
mipango ya kuifanya Yanga iwe klabu bora
Tanzania .
CHANZO NI YANGA FC
Tuesday, December 10, 2013
BENO , MAGARI WAULA YANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment