Tuesday, December 10, 2013

WANAUME WAWILI MASHOGA WAPATA VYEO VIKUBWA SEREKALINI...MMOJA NI WAZIRI MKUU MWINGINE MSAIDIZI


Hii itakua ya kwanza duniani kwa wanaume
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupata vyeo
vikubwa kwenye serikali kuu ya nchi.
Makundi mengi yenye maoni tofauti yamekuwa
yakipinga mapenzi ya jinsia moja na makundi
mengine yakitetea, huko Luxemburg mwanaume
anayejulikana kwa jina Xavier Bettel ambaye
ameweka wazi kwamba anashiriki mapenzi ya
jinsia moja amekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.
Hapo hapo mwanaume mwingine Etienne
Schneider ambaye pia aliweka wazi kuwa
anashiriki mapenzi ya jinsia moja amepewa
umakamo waziri mkuu akimsaidia kazi Xavier
Bettel .
Baada ya wawili hawa kupata vyeo hivi vya juu
imefanya nchi ya Luxemburg kuwa nchi ya
kwanza duniani kuwa na viongozi wa juu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja waziwazi.

1 comment:

.