Monday, December 9, 2013

BREAKING NEWSSSS ... MTOTO SULEIMAN RAJAB AFARIKI DUNIA GHAFLA


******
Na Imelda Mtema
MASKINI! Yule mtoto Suleiman Rajab
aliyeteseka muda mrefu akisumbuliwa
na uvimbe mkubwa mguuni huku
mamia ya Watanzania wakijitolea
kuchanga fedha kwa ajili ya matibabu
nchini India amefariki dunia ghafla
nyumbani kwao Ukonga-Kivule, Dar.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa
baada ya kifo hicho, baba mzazi wa
marehemu, Rajab Upinde alisema
kwamba mtoto wake huyo hakuwa
anasumbuliwa na kitu chochote zaidi ya
uvimbe uliokuwa mguuni lakini
alishikwa na ugonjwa wa ghafla na
kufariki dunia.
Baba huyo alisema kwamba Kampuni ya
Global Publishers kwa kushirikiana na
Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha
Mimi na Tanzania kwenye Runinga ya
Chanel Ten walifanya jitihada kubwa za
kukusanya michango ambayo
ilifanikisha maandalizi ya safari ya
matibabu India.
“Naumia sana kwa vile kila kitu kilikuwa
tayari. Tulikuwa tunasubiri siku ya
kuondoka tu. Global Publishers na Hoyce
wamefanya kazi kubwa kukamilisha
safari ya India lakini ndiyo hivyo Mungu
kampenda zaidi kiumbe wake,” alisema
baba huyo kwa uchungu.
Akizungumzia kifo cha mtoto wake, baba
huyo alisema kuwa siku ya tukio Sele
aliamka akilalamika kichwa kinamuuma
ambapo walimpa dawa za kutuliza
maumivu.
Alisema aliporejea kutoka kazini mkewe
alimwambia kuwa Sele alikuwa
akilalama kuwa miguu inawaka moto
ambapo alimfuata mwanaye chumbani
ambaye aliomba aitiwe shehe.Shehe
alipofika alimuombea na baada ya muda
aliwaita wadogo zake na kuwaambia
yeye anakufa kwani anajisikia vibaya
mno.
Baba huyo aliendelea kusema kuwa
akiwa amekaa nje alisikia mwanaye
mwingine akimuita aingie ndani kwani
hali ya Sele ilikuwa imebadilika na
alipoingia alimkuta mwili wote umelegea
ambapo aliita majirani ili wamsaidie,
walipoingia ndani walimkuta
ameshafariki dunia.Mungu ailaze roho
ya marehemu mahali pema peponi.
Amina.
“ Ki ukweli sikuweza kuamini macho
yangu kama mwanangu ndio ameniaga
kwani nilikuwa na ndoto nyingi za
kumuona akipona tena na kuwa mzima
kama walivyo watoto wengine” alisema
baba huyo.
Kampuni ya Global Publishers kwa
kushirikiana na kipindi cha Mimi na
Tanzania kinachorushwa kupitia
Televisheni ya Channel Ten na
mwanadada Hoyce Temu, na kwa
watanzania wote walio nje ya nchi kwa
kujitahidi kutoa michango yao Mungu
awabariki sana.

No comments:

Post a Comment

.