Itafanyika wapi? Costa do Sauipe, Bahia, Brazil
Kombe la dunia la mwaka 2014, linatarajiwa
kufanyika kuanzia tarehe 12 Juni hadi Julai kumi
na tatu.
Itakuwa mara ya 20 kwa kinyang’anyiro hicho
kuandaliwa huku ikiwa mara ya kwanza kufanyika
nchini Brazil tangu mwaka 1950 wakati wenyeji
waliposhindwa na Uruguay kwenye fainali.
Ijumaa hii mbivu na mbichi itajulikana na itakuwa
itakuwa wakati wa kujua nani atacheza na nani
katika kundi gani droo zitakapofanyika.
Droo yenyewe itafanyika kuanzia saa moja jioni
saa za Afrika Mashariki Ijumaa tarehe sita.
Itafanyika mjini Costa do Sauipe mkoani Bahia,
umbali wa maili 56 kutoka mjini Salvador, mji
utakaokuwa mwenyeji wa kombe hilo.
Wakati wa droo kutakuwa makundi manne
La kwanza likiwa na timu hizi: Brazil, Spain,
Argentina, Belgium, Colombia, Germany,
Switzerland, Uruguay.
Kundi la pili: Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria,
Cameroon, Chile, Ecuador.
Kundi la tatu: Japan, Iran, South Korea, Australia,
United States, Mexico, Costa Rica, Honduras.
Kundi la nne: Bosnia-Hercegovina, Croatia,
England, Greece, Italy, Netherlands, Portugal,
Russia, France.
Watakaofanya droo ni mchezaji wa zamani wa
England Sir Geoff Hurst, Zinedine Zidane wa
Ufaransa, Cafu wa Brazil na Fabio Cannavaro wa
Italia.
Timu 32 zilizofuzu zitawekwa katika makundi
manane kila kikundi kikiwa na timu nne.
Friday, December 6, 2013
Droo ya Kombe la dunia 2014 Brazil
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment