Friday, December 6, 2013

Wabunge Uganda wanunuliwa 'iPads'


Kumezuka malalamiko nchini Uganda baada ya
wabunge kununuliwa tabiti au (iPads) kwa pesa
za Umma.
Afisaa mkuu wa Bunge amesema kuwa tabiti hizo
zitawafanya wabunge kuwa makini wakati wa
vikao vya bunge.
Kamishna wa bunge Emmanuel Dombo amesema
kuwa wabunge sasa wanaweza kupata
stakabadhi zao rasmi wakati hata wakiwa nje ya
ofisi zao au wakiwa safarini.
Pia alisema kuwa pesa walizonunulia iPad hizo
zitasaidia kuepuka kutumia kiwango kikubwa cha
karatasi na kupunguza gharama ya matumizi.
Wabunge wote wa bunge la Uganda ambao idadi
yao ni 375, wanunuliwa zilizogharimu kima cha
dola laki tatu na sabini.
Wakosoaji wanahoji ikiwa wanasiasa wanajua
hata kuzitumia tabiti hizo na kusema kuwa tayari
wananchi wanalipa pesa nyingi sana kwa
mishahara ya wabunge
Mwaka jana wabunge wa Uganda walipiga kura
kutaka mishahara na marupurupu yao kuongezwa
kwa asilimia arobaini.
Pia walipokea marupurupu ya zaidi ya dola
40,000 ili kujinunulia gari jipya.
Mbunge wa Uganda kwa sasa hulipwa, dola elfu
nane , ingawa nchi hiyo inakumbwa na matatizo
ya kiuchumi.
Wananchi wanasema kua hatua hii ya serikali ni
kuharibu pesa za mlipa kodi, ikizingatiwa kuwa
wabunge hao wanalipwa mishahara ya juu
ambayo inawawezesha kujinunulia vifaa hivyo
wao wenyewe.

No comments:

Post a Comment

.