Monday, December 16, 2013

FUMANIZI LA LULU , YOUNG DEE UTATA


Stori: Musa Mateja na Mayasa Mariwata
MWISHONI mwa wiki iliyopita , taarifa zilienea
katika mitandao ya kijamii na vyombo
mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii
wa Bongo Fleva , David Genzi ‘ Young Dee ’ na
nyota wa filamu , Elizabeth Michael ‘ Lulu ’
wamebambwa na polisi wa doria wakivunja
amri ya sita ndani ya gari aina ya Hyundai,
Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio
lililojaa utata mkubwa .
Elizabeth Michael ‘Lulu ’ .
Kwa mujibu wa habari hizo , wawili hao
walinaswa wakifanya uchafu huo na askari
waliokuwa doria lakini wakawavuta chobingo
na baada ya muda , wakawaachia na
kutokomea kusikojulikana .
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la aibu,
paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya
Young Dee na kumsomea mashtaka yake
ambapo alifunguka kuwa ni kweli amezisikia
habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo
siyo ya kweli bali imezushwa na kundi la
watu wenye lengo la kumharibia jina lake
mbele ya jamii.
David Genzi ‘Young Dee ’.
“Siyo kweli kabisa , isitoshe nina kama mwezi
mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni
kutaka kuchafuliana majina tu , ” alisema
Young D .
Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee
kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa
muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja
ingawa hawakutaka kuonekana na mtu
yeyote .
Kwa upande wa Lulu alipotafutwa ,
alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama hiyo
ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni
kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi
nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka
kwenda popote , hata hiyo Mbezi iliyotajwa
mimi siielewi kabisa , hata lile gari mimi sina
gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda
gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu
sana sijaonana naye , ”
“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji
mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni,
nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo ?
Akanijibu kwamba amepata tetesi tu . Sasa
kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla
hajanichafulia jina?”
“Pia alisema kuna askari wa doria
walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho
kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe
kama ni kweli maana ishu hii inanichafua
mimi na familia yangu, akashindwa kufanya
hivyo .
“Yaani naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa
na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young
Dee maana kwanza hata sijawahi kukutana
naye hivi karibuni , sipendi kuchafuliwa na
haya yote namuachia Mungu atawajibu wote
wanaonizushia , ” alisema Lulu.

No comments:

Post a Comment

.