Stori: Gladness Mallya
MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini , Sara
Mvungi amefanyiwa kitu mbaya kwa
kukombwa vitu kibao kwenye bodaboda.
Sara Mvungi .
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi
jioni maeneo ya Kwanyerere , Mikocheni jijini
Dar es Salaam ambapo Sara alikuwa kwenye
bodaboda ghafla ilitokea nyingine ikiwa
kwenye mwendo wa kasi na wahusika
walikuwa wawili ambao walimnyang ’ anya
pochi.
Akizungumza kwa masikitiko, Sara alisema
ndani ya pochi hiyo kulikuwa na simu mbili
aina ya blackberry , fedha taslimu laki
tatu, dola mia moja , vitambulisho na vitu
vingine vingi .
“Nimeumia sana moyoni jamani sijui nianzie
wapi ila namshukuru Mungu sijaumia
nawaomba mashabiki na jamii kwa ujumla
kuwa makini kwani bodaboda siyo watu wa
kuaminika na huu mwisho wa mwaka ndiyo
wizi umezidi ,”alisema Sara .
Monday, December 16, 2013
SARA MVUNGI AFANYIWA KITU MBAYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment