Victoire Ingabire akiwa mahakamani
Mahakama ya juu zaidi nchini Rwanda
imeendeleza hukumu ya kwanza aliyopewa
kiongozi wa upinzani nchini humo Victoire
Ingabire na kuiongeza kutoka miaka 8 hadi 15.
Awali mwezi Oktoba, bi Ingabire ambaye ni wa
asili ya ki Hutu alipatikana na hatia ya ugaidi, na
kukana kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya
kabila la wa Tutsi.
Mauaji hayo yalifanyika mwaka wa 94 ambapo
zaidi ya watu 800 wa kabila la wa Tutsi
waliuawa.
Bi Ingabire alikata rufaa dhidi ya hukumu ya
awali aliyopewa japo upande wa mashtaka nao
ulitaka aongezewe hukumu hiyo na hata
kupendekeza apewe hukumu ya maisha gerezani.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty
International limeshutumu namna kesi ya Bi
Ingabire imeendeshwa.
Bi Ingabire amekumbwa na matatizo na sheria
ya Rwanda baada ya kurejea nchini humo
mwaka wa 2009, kutoka Uholanzi alikoishi kwa
miaka kadhaa. Alieleza wazi nia yake kuwania
urais nchini humo lakini hakupata fursa kwani
punde tu alipowasili alifunguliwa mashtaka hayo.
Kutokana na kujivuta kwa kesi yake, hakushiriki
uchaguzi uliofuata wa mwaka wa 2010. Tangu
wakati huo, amekuwa kizuizini. Amekuwa
akiwakilishwa na wakili kutoka Uingereza.
-BBC
Friday, December 13, 2013
HII KALI!!!! KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI RWANDA VICTORIE INGABIRE KUFUNGWA MIAKA 15 JELA....SOMA ZAIDI HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment