Thursday, December 5, 2013

Kapombe akwama. .. Dar , ashindwa kurudi Ufaransa


Aliyekuwa mchezaji kiraka wa Simba ,
Shomari Kapombe.
Na Khadija Mngwai
ALIYEKUWA mchezaji kiraka wa Simba,
Shomari Kapombe amejikuta katika wakati
mgumu kwa kushindwa kurudi Ufaransa
kutokana na kuchelewa kupata ruhusa ya
kuingia nchini humo .
Kapombe anaishi nchini Ufaransa ambako
anaichezea timu ya As Cannes inayoshiriki
Ligi Daraja la Nne ‘ Sefa ’ , lakini ameshindwa
kupata visa inayomruhusu kuingia tena nchini
humo .
Kapombe alirejea nchini kutokea Ufaransa
kwa ajili ya kuitumikia Taifa Stars katika
mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe , hivi
karibuni .
Kutokana na hali hiyo , Kapombe amekuwa
akionekana katika mitaa ya Dar es Salaam
akiendelea kupambana kupata visa hiyo
itakayomruhusu kurejea tena kazini .
Awali Championi Ijumaa lilikutana na
Kapombe katika ofisi za Shirikisho la Soka
Tanzania ( TFF ) na juhudi za kumhoji
kuendelea kuwepo nchini zilikwama baada ya
mmoja wa maofisa wa shirikisho hilo, Saad
Kawemba kuzuia kwa juhudi kubwa
asizungumze .
Kawemba , huku akiwa amenuna , alimuambia
Kapombe: “Twende twende Kapombe.”
Akionyesha kumzuia asihojiwe, naye hakuwa
na ujanja , akatekeleza agizo hilo la kibabe . ”
Lakini baadaye , Kaimu Katibu Mkuu wa TFF ,
Boniface Wambura akaonyesha ukomavu na
kutoa ushirikiano kwa kuweka mambo wazi
na kusema tatizo la Kapombe ni visa .
“Kapombe yupo hapa nchini kutokana na visa
yake kwisha muda , aliyokuwa nayo ni ya
muda mfupi . Ilikuwa inamruhusu kubaki
Ufaransa na akitoka tu , imekwisha na
anatakiwa kupata nyingine .
“Kwa sasa haruhusiwi kurejea kule hadi
apate visa mpya , TFF na AS Cannes
tumekuwa tukishirikiana ili kumuwezesha
kurejea tena kazini mapema , ” alisema
Wambura aliyeonyesha ushirikiano .
Tayari Kapombe alipata uhakika wa kuanza
kucheza katika kikosi cha kwanza cha AS
Cannes baada ya kurejea akitokea katika
majeruhi .

No comments:

Post a Comment

.