Thursday, December 5, 2013

TANZANIA YAPATA MGAO WA TIKETI 260 ZA KOMBE LA DUNIA.


Muonekano wa uwanja ambao utachezewa kombe
la dunia huko Brazil
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) limeipa Tanzania mgawo wa tiketi 260
za Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Watanzania wanaohitaji tiketi hizo
wanatakiwa kutuma maombi TFF kwa
maandishi wakielezea aina ya tiketi na mechi
wanazotaka kushuhudia. Hakuna tiketi
zitakazoombwa FIFA bila kuwepo maombi
kwa maandishi.
Tiketi zilizopo kwa Tanzania ni ifuatavyo;
kwa hatua ya makundi (ukiondoa mechi ya
ufunguzi), raundi ya 16 bora, robo fainali na
mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ni 250.
Kwa mechi ya ufunguzi, nusu fainali mbili na
fainali (mechi namba 1, 61, 52 na 64) ni tiketi
kumi tu ndizo zitakazopatikana. Bei za tiketi
ziko katika viwango vitatu tofauti.
Mechi ya ufunguzi tiketi zake ni dola za
Marekani 495, 330 na 220. Hatua ya makundi
(mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90.
Hatua ya 16 bora (mechi namba 49-56) ni
dola 220, 165 na 110.
Robo fainali (mechi namba 57-60) ni dola
330, 220 na 165 wakati nusu fainali (mechi
namba 61 na 62) ni dola 660, 440 na 275.
Mechi ya mshindi wa tatu ni dola 330, 220
na 165. Kiingilio kwa fainali kitakuwa dola
990, 660 na 440.
TFF itawasilisha maombi ya tiketi hizo FIFA
kuanzia Desemba 8 mwaka huu hadi
Februari 7 mwakani. Idadi ambayo itaombwa
FIFA itatokana na Watanzania waliowasilisha
maombi TFF kwa vile zinaweza zisipatikane
tiketi zote hizo zilitengwa kwa Tanzania.
Hivyo tunasisitiza maombi ya tiketi
yatakayofanyiwa kazi ni yale ambayo
yamewasilishwa TFF kwa maandishi tu.
Reactions:

No comments:

Post a Comment

.