Na Martha Mboma
KIUNGO mshambuliaji wa Ashanti United,
Said Maulid ‘ SMG ’ , amesema kutua kwa
kocha Abdallah Kibadeni katika timu yao,
kutaleta mabadiliko makubwa katika
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Kibadeni amejiunga na timu hiyo katika
maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi
baada ya uongozi wa Simba kumtimua yeye
na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘ Julio’ .
Akizungumza na Championi Jumatano , SMG
alisema kocha huyo ana uzoefu mkubwa wa
kufundisha soka , hivyo anaamini ataipa
mafanikio makubwa timu hiyo .
SMG alisema anaamini kuwa timu yao
itakuwa na mabadiliko makubwa kutokana na
uwezo wa kufundisha wa kocha huyo.
“Ni kocha mzuri mwenye heshima kubwa
nchini kutokana na uwezo wake wa kufanya
kazi, ataisaidia timu yetu hasa katika
upungufu tuliokuwa nao katika mzunguko wa
kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara .
“Benchi la ufundi baada ya kuwasilisha ripoti
yao, nina imani watayafanyia kazi yale
yaliyoainishwa ili kujipanga zaidi ili
kukiimarisha kikosi hiki , ” alisema SMG .
Tuesday, December 10, 2013
Kibadeni ampa SMG jeuri Ashanti United
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment