Tuesday, December 10, 2013

Coastal yakimbilia Oman


TIMU ya Coastal Union imepanga kucheza
mechi tano pekee za kirafiki ndani na nje ya
Tanzania katika kujiandaa na mzunguko wa
pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza
Januari, mwakani.
Coastal ambayo imemalizia mzunguko wa
kwanza ikiwa katika nafasi ya nane, inaingia
katika mzunguko wa pili ikiwa na kocha
mpya kutoka Kenya, Yusuf Chipo, ambaye
anaanza kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza na Championi Jumatano ,
katibu wa timu hiyo , El Siag Kassim , alisema
lengo la mechi hizo ni kuwaandaa wachezaji
wao , pia kuzoeana kabla ya kuanza
mzunguko wa pili wa ligi .
Kassim alisema timu hiyo wakati wowote
itaelekea nchini Oman kwa ajili ya kuanza
kambi ya pamoja kujiandaa na mzunguko
huo wa pili kwa kucheza mechi mbalimbali
za kirafiki .
“Timu yetu itacheza mechi tano za kirafiki
ambazo zitachezwa ndani na nje ya
Tanzania ili kujipima na kujiimarisha zaidi
katika mzunguko wa pili wa ligi kwa kufanya
vizuri zaidi , ”alisema Kassim.

No comments:

Post a Comment

.